Video
ya msanii Faustina Charles maarufu Nandy inayomuonyesha akiwa faragha
na mwanaume leo imezua gumzo mitandaoni ambapo mwenyewe amefunguka.
Nandy amekiri kwamba video hiyo ni ya kweli japo ni ya mwaka 2016 na kuwaomba Watanzania na Serikali msamaha kwa walichokiona.
Akielezea
zaidi, amesema video hiyo ilichukuliwa akiwa katika uhusiano na mmoja
wa wasanii wa Bongo Fleva (jina tunalihifadhi), ambapo walikubaliana
yawe ya siri.
“Sielewi
ana maana gani kuitoa video hiyo kwa sasa na kufika kwenye mitandao,
kwani ni vitu kama hivi vinafanyika kwa mtu yeyote anayekuwa kwenye
mahusiano,” amesema.
“Nimesikitishwa
sana na kitendo hicho na ‘ilishutiwa’ kwa mtindo wa ‘Snapchat’ na sijui
kwa nini ameamua kuirushia sasa hivi, yaani sielewi nifanye nini.”
“Naomba
radhi kwa mashabiki wangu, familia yangu, kanisani kwangu, Serikali
kiukweli video imenichafua sana ila adhabu ya maumivu haya ninayoyapata
sasa hivi ni kutokana na kumuamini mtu.”
“Sina
cha kusema kwani hiki siyo kitu cha kwanza, kwani ni’shakuwa na
mahusiano na mtu huko nyuma na akatishia kutoa picha zangu mpaka pale
nilipoenda kuripoti polisi.”
Hata hivyo, Nandy amewaasa vijana kuwa waangalifu wanapokuwa katika uhusiamo kwani tukio hilo wengi wamelichukulia kama ‘kick’.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni