Na Agness Francis, Blogu ya Jamii
RAIS
 wa Serikali ya Awamu ya Tano Dk. John Mgufuli  kuwa mgeni rasmi katika 
maadhimisho ya uhuru wa habari  Nchini ambayo kitaifa yatafanyika Mkoani
 Dodoma  Mei 2 hadi 3  mwaka huu ikiwa ndio kilele chake na kauli mbiu 
inasema  ni wajibu wa Serikali vyombo vya habari haki na utawala wa 
sheria.
Ambapo 
 wageni  zaidi ya 300 wanatajiriwa kuhudhuria  hafla hiyo wakiwepo wadau
 , wanahabari  ,wabunge na taasisi mbalimbali ambapo kimataifa Afrika  
inafanyika Nchini Ghana Accra zaidi ya nchi 100  zitawakilisha katika 
hafla hiyo.
Akizungumza 
 jjjini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Taasisi  ya vyombo vya habari Kusini
 mwa Jangwa la Sahara Salome Kitomari amesema katika siku hizo 
watazungumzia umuhimu wa  uhuru wa habari, utawala bora kwa waandishi wa
 habari na  wanasheria kama Mahakama kuwa na uhuru  wa kusimamia kesi za
 jinai za kuwa na uwazi kwa wanahabari vilevile na kukumbusha kutekeleza
 majukumu katika  uandikaji wa habari kuwa sahihi.
Aidha
 Makamo wa Rais wa Umoja wa Klabu za waandishi wa habari Jane Mihanji 
amesema wao wamekuwa na jukumu la kuwaweka pamoja waandishi wa  habari  
na kuwapa mafunzo na  kuwapatia  vitendea kazi.
Ametaja
 baadhi ya vitendea kazi hivyo ni kamera na kompyuta  ili kurahisishia 
majukumu yao ya kuhabarisha umma ambapo amesisitiza kutokana na uhaba wa
 vyumba vya habari  mikoani  inakuwa vigumu kupata stori kutoka nje ya 
Dr es Salaam.Hivyo amesema wamewajengea uwezo  wa mafunzo  ili 
kuhakikisha mazingira ya kazi yanakuwa rafiki katika utendaji.
"Tumeshuhudia
 stori ikiwa inatoka lakini katika kufufua maovu yanayotendeka  inaleta 
 misukosuko, hivyo tunaomba Serikali kuwajibika kufanya kazi yake kwenye
 upande wa haki na waandishi wa habari kutoa taarifa bila kupendelea mtu
 na kutoa chukua rushwa,"amesema Mahinja.
Mkurugenzi
 wa  Tanzania Media Foundation (TMF) Fausta Musokwa amesema 
watashirikiana na wadau wengine kwenye tasnia ya habari kuadhimisha siku
 hiyo umuhimu na wapo kwa ajili ya kuimarisha vyombo vya habari 
vinafanya kazi katika mazingira rafiki na kuhakikisha wanahabari kutoa 
taarifa makini zenye ubora  kwa  jamii.
Kwa
 upande wa Ofisa habari wa Umoja wa  Wataifa (UN) Stella Vuzo amesema 
kwa sasa umoja huo unatekeleza maendeleo  endelevu ifika 2030 kila nchi 
hupaswa kuelezea namna gani imetekeleza hilo lengo na kuhakikisha kuwepo
 na ushirikiano kwa wanahabari kusaidia kupata taarifa mbali mbali .
Mwenyekiti
 wa MISA Tanzania Bi. Salome Kitomari akizungumza na waandishi wa habari
 kuhusu maandalizi ya maadhimisho ya uhuru wa habari  Nchini ambayo 
kitaifa yatafanyika Mkoani Dodoma  Mei 2 hadi 3  mwaka huu na kauli mbiu
 inasema  ni wajibu wa Serikali vyombo vya habari haki na utawala wa 
sheria.
Makamu
 wa Rais wa  Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Jane
 Mahanji akizungumza na waandishi wa habari namna wanavyokwenda 
begakwabega na waandishi kwa kuto semina ili kutoa habari zenye faida 
kwa Taifa.
Mkurugenzi
 wa  Tanzania Media Foundation (TMF) Fausta Musokwa akizungumza na 
waandishi wa habari wanavyochangia kwa kiasi kikubwa vyombo vya habari 
kwa kutoa pesa ili vyombo hivyo vijiendeshe.
Afisa
 Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo 
akizungumza na waandishi wa habari kuhusuumoja wa Mataifa unavyodhamini 
mchango mkubwa wa waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi wa 
habari kuelekea siku ya uhuru wa vyombo vya habari hapa nchini.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni