Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia), Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura (wa pili kushoto) pamoja na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez (kulia) wakiwasha mishumaa wakati wa tendo la Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari yaliyoadhimishwa leo Aprili 7, 2018 kwenye ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Mlimani City jijini Dar es Saalam.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
LEO April 7 raia wa Rwanda waishio nchini Tanzania wameadhimisha miaka 24 ya mauaji ya kimbari yalipoteza zaidi ya watu milioni moja kwa siku 100 hasa kabila la Watutsi na kuacha yatima, wajane wengine wengi katika hali ngumu. Raia hao wameeleza kuwa kilichotokea hawatakisahau na hakitatokea tena.
Mgeni rasmi katika kumbukizi hizo Waziri wa Habari, sanaa vijana Utamaduni na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe ameeleza kuwa tukio hilo ni la kusikitisha sana hata Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli alipofanya ziara nchini Rwanda mwaka 2016 alitembelea kituo cha mauaji hayo huko Kigali na kueleza kuwa haya yalianza kwa kupandikiza chuki katika jamii na kusisitiza kuwa mauaji haya hayatatokea tena Rwanda na kwingineko Afrika.
Aidha Mwakyembe ameeleza kuwa lazima tusaidiane na kushirikiana ili kuhakikisha haya hayatokei tena barani Afrika.
Naye Balozi wa Rwanda nchini ameeleza kusikitishwa na tukio hilo ambalo liliathiri wananchi na taifa kwa ujumla lakini baada ya vita Rwanda iliungana tena na kuwa wamoja na kuleta maendeleo, ameeleza kuwa wanawakumbuka wenzao ambao walilengwa kuuawa na hawatasahaulika kamwe. Pia hadi sasa wananchi wameungana pamoja na wapo sambamba katika kuleta maendeleo nchini humo.
Naye Mwakilishi wa umoja wa mataifa (UN) Alvaro Rodriguez ameeleza kuwa waliouawa watakumbukwa Rwanda na kueleza kuwa kuokoa maisha ya watu lazima kuwe na matendo na katika kuelekea maadhimisho ya miaka 70 ya haki za binadamu lazima kila nchi ijizatiti katika kutimiza malengo yake ya kulinda haki za binadamu.
Maadhimisho hayo yalianza kwa sala fupi na baadaye mishumaa kuwashwa kama ishara ya kuwakumbuka wenzao waliouwawa kwenye mauaji hayo.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura pamoja na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez wakiwasha mishumaa pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Shule za Sekondari za Kimasila na Chang'ombe wakati wa tendo la Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari yaliyoadhimishwa leo Aprili 7, 2018 kwenye ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Mlimani City jijini Dar es Saalam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni