SeeBait
Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka label ya WCB Harmonize kwa mara ya kwanza amefungukia suala la kuvunjika kwa Mahusiano ya Zari na Diamond Platnumz.

Miezi miwili iliyopita siku ya wapendanao Zari alitumia ukursa wake wa Instagram kumwaga aliyekuwa mpenzi wake Diamond baada ya kuzidisha michepuko ingawa suala hilo lilitokea muda mrefu uliopita lakini mpaka leo linatrend.

Harmonize mbali ya kuwa msanii wa Diamond lakini pia ni mtu wa karibu ambaye pia alikuwa na ukaribu na Zari kwaiyo alipoulizwa anachukuliaje wawili hao kuachana alisema anaheshimu maamuzi ya Zari.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Funiko Base ya Radio Five, Harmonize amefunguka na kusema kuwa yeye binafsi anaheshimu maamuzi ya Zari kwa sababu ana maamuzi yake binafsi.

"Mimi naheshimu sana maamuzi ya mtu siwezi kuongea kama ni vibaya au ni vizuri Kwanza muda wa kumshauri mtu kuhusu Mahusiano Yake ndio sina”.

Lakini pia Harmonize alisisitiza kuwa hawezi kumuongelea sana Zari na kuorodhesha mambo ambayo alimsaidia kwani unaweza ukaonekana mnafki.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni