Na Mahmoud Ahmad Dar.
Mkuu wa mkoa wa Dar
es Salaam, Mhe Paul Makonda ameongeza
siku tano zoezi la kuwapatia msaada wa kisheria wakina mama
waliotelekezwa na
waume zao,ambapo amesema kwanzia wiki ijayo wataanza kusikilizwa wakina
baba wanaolalamikiwa pamoja na kuwasikiliza wakina mama waliobakia na
kuwataka wanaume watakaoitwa wafike bila kukosa ili
kuepusha kutajwa majina yao hadharani.
Rc
Makonda amesema wanaume watakaopewa wito wa kufika
ofisini kwake wasikaidi kwani atakayeshindwa kufika jina lake litatajwa
hadharani, na pia amewapongeza wakina baba waliokubali wito na kusema
kuwa kwanzia wiki ijayo
wakina baba wanaolalamikiwa wataanza kufika kwa ajili ya upatanishi.
"Wakina baba wanaolalamikiwa waliopewa wito wataanza
kufika kwanzia jumatatu ya wiki ijayo kwa ajili ya upatanishi na wale
watakaokaidi tutataja majina yao hadharani hivyo wakina baba watakaokaidi kuja
kwa ajili ya kupatanishwa nitawatangaza majina yao hadharani"Amesema Makonda.
Aidha amesema wapo watu wanaobeza zoezi hilo katika mitandao
na kuona ni jambo la Faragha,ambapo amesema lengo la zoezi hilo siyo kumuumbua mtu bali ni kutafuta haki ya kila mtoto na kuondokana na watoto omba omba walioko
mitaani.
"Nyie mlioko nyumbani mnahaki ya kubeza hili zoezi nmna
haki ya kuandika mnachoandika lakini mimi namtazama mama anayeteseka, kwaiyo waache waseme wanachokisema lakini
mimi furaha yangu ni amani ya watoto na kina mama wanaoteseka"Amesema Rc
Makonda.
Amesema zoezi hilo lina faida kwa wakinamama wote hata
walioko kwenye ndoa kwani litasaidia kuwapatia haki watoto wote na kusaidia
watoto kufahamika katika familiya na kubainisha kuwa hii itasaidia kupunguza
wakina dada wanaowaza kutoa mimba ama kutupa watoto wachanga.
Pia amewaasa wakina mama na
wanawake wote wa mkoa huo kutumia kinga wakati wanapofanya tendo la ndoa ili
kupunguza kasi ya Ugonjwa wa UKIMWI kwani kwa kipindi kifupi ugonjwa huo
umeongezeka kwa asilimia 45% kwa watoto wenye umri chini ya miaka 24.
"Tunataka katika mkoa huu kina dada wasiwaze kutoa
mimba, wasiwaze kutupa kichanga na wanaume wanaopanga kuwapa mimba mwanamke
kama ajajipanga aogope kama ilivyo kubaka"Amesema.
Kwa
upande wao kina Mama waliofika kupatiwa huduama wamemshukuru Rc Makonda
kwa kutambua na kuona kilio chao ambapo wameshangazwa na watu wanaobeza
zoezi hilo ambalo wanaona limewasaidia kupata haki zao na za watoto
wao.
Tokea kuanza kwa zoezi la kuwasikiliza wakina mama waliotelekezwa na
kupatiwa msaada wa kisheria zaidi ya kina mama 10,000 wamefika kupata huduma na kati yao wanawake 4,000
wamesikilizwa na Familiya 205, wamekubali kwa maandishi kuwahudumia watoto wao na wengine 21 wamepimwa DNA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni