NYUMBA ZA POLISI ZIMENIPA MKE JANETH-RAIS MAGUFULI


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Maguli amesema jeshi la polisi ndilo lilimpa mke aliye naye  sasa, Mama Janeth Magufuli ambaye baba yake alikuwa ni polisi mpaka alipofariki dunia.
Rais ameyasema hayo leo Jumamosi, Aprili 7, 2018 baada ya kuzindua kituo cha polisi cha Kidiplomasia na Utalii  eneo la Naura Jijini Arusha na baadaye nyumba 31 za polisi zilizojengwa kwa ushirikiano wa serikali na wafanyabiashara baada ya zilizokuwepo kuungua moto Septemba mwaka jana.

“Nyumba za polisi nazifahamu vizuri sana, ndiyo zilizonipa mke, huyu mke wangu baba yake alikuwa polisi, na mpaka amekufa wala hakuwa na cheo, alikuwa ‘staff sergeant’, kwa hiyo maisha ya polisi ninayafahamu na yamenitunzia mke.
“Ningekuwa nazindua nyumba kama hizi huko Moshi, angenionyesha nyumba walizoishi lakini za Oyster Bay alizoishi alishanionyesha na za Ukonga na za sehemu nyingine. Kwa hiyo maisha ya polisi ninayafahamu. Kwa hiyo polisi mna msemaji mwingine ambaye ni mke wangu ukiachilia mbali Waziri wa Mambo ya Ndani (Mwigulu) na IGP Sirro,” amesema Rais Magufuli.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni