Mkuu wa
Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amefiwa na mama yake mzazi usiku wa kuamkia
leo katika hospitali ya The Madras Medical Mission – Chennai nchini
India alipokuwa akipatiwa matibabu.
RC Gambo
kupitia mtao wake wa Instagram amethibitisha kifo hicho huku akieleza
kuwa anahiaji maombi kwasababu huo ni mtihani mzito sana kwake.
"Kwa
masikitiko na uchungu mkubwa napenda kutangaza kifo Cha Mama yangu Mzazi
( Mama aliyenilea kwa kuuza uji) kilichotokea usiku wa leo kwenye
hospitali ya The Madras Medical Mission – Chennai nchini India!
"Kama
mtoto nilijitahidi kufanya kila lililowezekana ikiwa ni pamoja na
kumpeleka Afrika Kusini kwa matibabu kabla ya India. Ni Imani yangu kuwa
hata Mungu atakubali kuwa kama binadamu nilifanya kila lililowezekana
Ila yeye kampenda zaidi! Niombeeni sana maana mtihani huu ni mzito sana
kwangu sidhani kama nita uhimili!"
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni