Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo TANZIA. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo TANZIA. Onyesha machapisho yote

TANZIA: MBUNGE MAJIMAREFU AFARIKI DUNIA



MBUNGE wa Korogwe Vijijini (CCM) mkoani Tanga,  Steven Ngonyani maarufu Profesa Majimarefu amefariki dunia leo Jumatatu Julai 2,  2018 usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Taarifa za kifo cha mbunge huyo zimethibitishwa na ofisa uhusiano wa Muhimbili, Aminiel Eligaeshi.
Juni 20,  2018 Majimarefu alihamishiwa kwa ndege kutoka mkoani Dodoma kwenda MNH kwa matibabu huku ugonjwa uliokuwa ukimsumbua mbunge huyo haujawekwa wazi.
Juni 6,  2018 mbunge huyo alifiwa na mkewe,  Mariam aliyekuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali hiyo hiyo ya Muhimbili.

JUMUIA YA CHUO KIKUU CHA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI MUHIMBILI YAMUAGA MAREHEMU PROF. LEONARD LEMA


Wanataaluma wakiongozwa na Mkuu wa Idara ya Upasuaji wa MUHAS wakiandamana kusindikiza mwili wa marehemu Prof. Leonard Lema kuelekea graduation square, MUHAS kwa ajili ya tukio la kumuaga mwanataaluma mwenzao.
Viongozi mbalimbali wa MUHAS, MNH, MOI na JKCI wakisimama kwa heshima wakati mwili wa marehemu Prof. Leonard Lema ukiwekwa vizuri tayari kwa tukio la kumuaga
Mkuu wa Idara ya Upasuaji, MUHAS, Dkt. Larry Akoko akisoma wasifu wa marehemu maru tu baada ya mwili kuwasili kwenye graduation square MUHAS.
Viongozi mbalimbali taasisi na vyama vya kitaaluma wakitoa salamu za rambirambi wakati wa tukio la kuaga mwili wa Prof. Lema
Mke wa marehemu pamoja na watoto wake mara baada ya kupokea Tuzo ya Heshima iliyotolewa na Chama cha Madaktari Bingwa wa Upasuaji Tanzania, kwa marehemu Prof. Leonard Lema kwa kutambua mchango wake katika kuendeleza Taaluma ya Upasuaji nchini. Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili Prof. Appolinary Kamuahabwa akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Lawrence Museru wakipita kuaga mwili wa marehemu Prof. Leonard Lema.
Mke wa marehemu pamoja na watoto wake mara baada ya kupokea Tuzo ya Heshima iliyotolewa na Chama cha Madaktari Bingwa wa Upasuaji Tanzania, kwa marehemu Prof. Leonard Lema kwa kutambua mchango wake katika kuendeleza Taaluma ya Upasuaji nchini.
Wanataaluma na wafanyakazi wengine wa sekta ya afya akiaga mwili wa marehemu Prof. Leonard Lema katika eneo la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, MUHAS
Familia ya marehemu ikiaga mwili wa mpendwa wao Prof. Leonard Lema katika eneo la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, MUHAS
Familia ya marehemu ikiaga mwili wa mpendwa wao Prof. Leonard Lema katika eneo la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, MUHAS

Chuo Kikuu cha afya na Sayansi Shirikishi Muhmbili (MUHAS) pamoja na jumuia yote ya Hospitali ya taifa ya Muhimbi (MNH), Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo wameaga mwili wa marehemu Prof. Leonard Ellisa Lema, katika eneo la graduation square, MUHAS.

Tukio hili la kuaga mwili wa marehemu Prof. Lema lilitanguliwa na maandamano ya wanataaluma ili kumuenzi mwanataaluma mwenzao kwa mchango wake katika taaluma.

Pamoja na kutoa salamu za pole kwa familia ya marehemu kwa kuondokewa na mpendwa wao, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Appolinary Kamuhabwa alisema marehemu Prof. Leonard Lema atakumbukwa kwa moyo wake wa kujituma na kuchapa kazi kwa juhudi, maarifa na nidhamu. "Chuo na Taifa kwa ujumla limempoteza mtu ambaye alitoa mchango mkubwa katika sekta za Elimu ya Juu na Afya nchini hasa katika fani ya huduma za upasuaji" aliongeza Prof. Kamuabwa.

Pia katika tukio hili Chama cha Madaktari Bingwa wa Upasuaji Tanzania, kimemtunukia marehemu Prof. Leonard Lema Tuzo ya Heshima kwa kutambua mchango wake katika kuendeleza Taaluma ya Upasuaji nchini. Tuzo hii ilikabidhiwa kwa Mke wa Marehemu.

RC Gambo afiwa na Mama yake


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amefiwa na mama yake mzazi usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya The Madras Medical Mission – Chennai nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.

RC Gambo kupitia mtao wake wa Instagram amethibitisha kifo hicho huku akieleza kuwa anahiaji maombi kwasababu huo ni mtihani mzito sana kwake.

"Kwa masikitiko na uchungu mkubwa napenda kutangaza kifo Cha Mama yangu Mzazi ( Mama aliyenilea kwa kuuza uji) kilichotokea usiku wa leo kwenye hospitali ya The Madras Medical Mission – Chennai nchini India! 

"Kama mtoto nilijitahidi kufanya kila lililowezekana ikiwa ni pamoja na kumpeleka Afrika Kusini kwa matibabu kabla ya India. Ni Imani yangu kuwa hata Mungu atakubali kuwa kama binadamu nilifanya kila lililowezekana Ila yeye kampenda zaidi! Niombeeni sana maana mtihani huu ni mzito sana kwangu sidhani kama nita uhimili!"

Alichosema Mama Kanumba katika Kanumba Day


SeeBait
Wadau wa tasnia ya filamu na familia ya marehemu Steven Kanumba, leo wanaadhimisha miaka sita tangu kufa kwa msaanii huyo.

Mama yake Flora Mtegoa, amesema yeye kwake msiba huo bado upo kila siku na kudai kila nafsi itaonja mauti.

Mtegoa ameyasema hayo leo Aprili 7 katika makaburi ya Kinondoni ambapo walifanya ibada fupi kwa ajili kumbukumbu hiyo akiwa na baadhi ya wasanii hususani wa kikundi cha Soweto ambao ndio wameisimamia shughuli hiyo kwa mwaka huu.

Amesema pamoja na kujitokeza kwa wasanii wachache ambao waliwahi kufaya kazi na mtoto wake enzi za uhai wake anaamini ni kutokana na wao kuona wameshamaliza msiba, lakini kwake upo kila siku na kamwe hauwezi kufutika mpaka mwisho wa uhai wake.

"Ni kweli idadi ya wasanii maarufu waliokuja hapa ni wachache ukilinganisha na namna Kanumba alivyoishi nao, lakini ndio hivyo huwezi kuwalazimisha na isitoshe wao labda wanaona wamemaliza msiba lakini kwangu bado upo ila ninachowaombea yasije yakawakuta kama haya ndio watajua nini namaanisha,’’ amesema Mama Kanumba.

Wito wake kwa wasanii Mama Kanumba amewashauri kuwa na upendo kauli ambayo Kanumba alikuwa anapenda kuisema enzi za uhai wake.

TANZIA: DKT AMAN WALID KABUROU NA MANJU MSAMBYA


Inna lillah wainna Illah rajiun.Poleni wana Ujiji poleni wana Kigoma poleni wana CCM na poleni Watanzania.

Ilikuwa alfajiri ya leo saa 12.37 asubuhi nilipopokea simu kutoka rafiki na ndugu yangu Ahmed Maaruf Byemba almaarufu Yaounde. Alianza na kauli niliyoanza nayo hapo juu. 

Nikajua yametimia kwani ndugu yangu huyo anamuuguza mdogo wake kule Dodoma hivyo nikaelewa mgonjwa wake amefariki. Haikuwa hivyo bali alikuwa ananifahamisha kuwa Dk. Aman Walid Kaburou hatunae tena.

Niliduwa japo sikushangaa kwani taarifa za ugonjwa nilikuwanazo na hata taarifa za kupekekwa Muhimbili kutokea hospitali ya Maweni Kigoma nilikuwanazo na ndio maana sikushangaa. Ila niliduwaa kutokana na ninavyomfahamu Dk Kaburou. Nina historia nae.

Baada ya kupata maelezo toka kwa ndugu Yaounde nakuondokana na mduwao uliokuwa umenipata niliendelea kupata simu kuhusiana na kufariki kwa Dk Kabourou kutoka kwa ndugu wengine, hususan wana Ujiji.

Kifo cha Dk Aman Walid Kabourou kimenirejesha kifikra zaidi ya miaka 68 tokea sasa tukiwa watoto hadi kipindi cha kuanza elimu ya msingi. Mimi nilikisoma Ujiji Government Town School na Aman akiwa Kipampa Lower Primary School.

Sote tulikutana Kipampa Middle School mwaka 1962.Tulisoma hapo kwa miaka minne hadi tulipohitimu darasa la nane mwaka 1965 na kujiunga na elimu ya sekondari pale Livingstone College mwaka 1966.

Kifo cha Dk Kabourou kimenikumbusha mikimiki ya pale Livingstone hadi kusababisha kukatiza masomo tukiwa tumehitimu kidato cha tatu tu. Hapa leo sio mahala pa kuelezea hiyo mikimiki bali kumuomboleza Dk Aman Kabourou.

Baada ya kutoka shule hiyo 1968, mimi nilielekea Dar es Salaam kutafuta maisha ambapo mwezi Mei 1969 nilipata ajira ya muda Shirika la Reli la Afrika Mashariki(EARC) wakati nasubiri kwenda Nairobi, Kenya kuchukua mafunzo ya Ufundi Mitambo ngazi ya cheti mwaka uliofuata. Jambo lililofanikiwa kwa msaada wa Mhandisi Juma Omari Lweno aliyekuwa Mhandisi Mitambo (Mkoa wa Tanzania). Ikumbukwe nilikuwa nimeishia kidato cha tatu hivyo mafunzo hayo yalinichukua miaka minne ikijumuisha miaka miwili ya mafunzo kwa vitendo.

Wakati mimi nashughulika na ajira na mafunzo, Aman alibaki Ujiji akimsaidia baba yake katika biashara ya nguo za mitumba. Hapa ni vyema kutambua kuwa enzi zile nguo za mitumba zilikuwa zinaingizwa Tanzania kutokea Burundi pamoja na kwamba ilikuwa inapitishiwa bandari ya Dar es Salaam. Kwa ufupi nchini Tanzania miaka ya katikati ya 1960s hadi ile ya 1980s nguo za mitumba zilikuwa zinauzwa kiuficho.

Mwaka 1972 nilirejea Dar es Salaam kwa ajili ya muhula wa kwanza wa mazoezi kwa vitendo. Kwa urahisi wa kuwa jirani na karakana (Kituo Cha Reli, Dar es Salaam) nilipanga chumba Mtaa wa Aggrey, nyumba Na 97 ambayo ndugu Bakhresa baadae aliinunua na hivi sasa ni moja ya ofisi au maeneo ya shughuli zake.

Wakati nikiishi hapo na kama kumbukumbu zangu zinaniongoza vizuri, mwishoni mwa mwezi Machi, 1972 ndugu Aman aliamua kuachana na biashara ya mitumba akaja Dar es Salaam tukaishi pamoja (chumba hicho hicho kimoja). Lengo lake likiwa kutaka kujiendeleza kielimu.

Alipokuja kujiunga nami pale Aggrey, ndugu Aman alinikuta nahudhuria masomo ya jioni kwenye Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Lumumba (kwenye jengo kilpoanzia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam). Pale niliamua kusoma mambo matatu ambayo ni masomo ya "O Leval" ambayo nilikatizwa shuleni nakufanya mtihani wa "London GCE" ambao nilifanyia Nairobi huku nikiebdelea na masomo ya Reli. Pia nilikuwa najifunza "Creative Writing" iliyonisaidia katika masomo ya stashada (Diploma ya Uandishi wa Habari ambayo nilihitimu Novemba 1976. Kadhalika nilijifunza Kifaransa lugha ambayo nilijifunza hadi Chuo Kikuu.

Ndugu Aman alifurahishwa sana aliponikuta najiendekeza kielimu. Nakumbuka aliwahi kuniambia kwamba ni lazima tujielimishe ili tuthibitishe kuwa kule Livingstone College hatukwenda kwa bahati mbaya na kwa yeyote aliyetufitini ajiulize kwa nini alifanya hivyo.

Ndugu Aman alilenga kusoma nje ya nchi. Hivyo kila siku asubuhi hadi saa mbili usiku (Jumatatu hadi Ijumaa) alishinda Maktaba ya Taifa akijisomea mambo mbali mbali ya utashi wake. Ni huko Maktaba ya Taifa ndiko kulikopatikana njia yakuelekea kupata shahada ya Uzamivu (Ph D).

Akiwa "mwanafunzi" wa maktaba alikutana na Wamarekani Weusi ambao walimuomba awafundishe Kiswahili;na katika kutekeleza hilo waliweza kumpatia wepesi wakwenda kuishi Marekani kupitia Ethiopia na Italia.

Ndugu Aman aliondoka nchini Oktoba,1972.

Kabla hajaondoka aliniusia haya "MZEE MSAMBYA (pamoja na umri wetu mdogo na wa ujana miaka ile alipenda kuniwakilisha kwa heshima ya Mzee na amekuwa akinichukulia hivyo maisha yake yote) INABIDI TUPATE ELIMU KWA NAMNA YEYOTE ILI NASISI TUWE SEHEMU YA UONGOZI WA NCHI YETU.

Na imekuwa hivyo maana sote tumekuwa wabunge (yeye Kigoma-Ujiji) mimi Kigoma Kusini.Dk Kabourou aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Chadema(Taifa)na hivi karibuni alikuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma. Kwa upande wangu nimewahi kuwa Naibu Waziri (Nishati & Madini) na takriban miaka miwili nyuma nilikuwa Mkuu wa Wilaya. Hizo ni nafasi za uongozi kama alivyobashiri Ndugu Aman Walid Kabourou.

Nikiri kuwa kuishi kwangu pamoja nae ule mwaka 1972 kulikuwa chachu ya baadhi ya mafanikio yangu.

Ndugu Aman baada ya kuhitimu shahada ya Uzamivu (Ph D) alifanyakazi Marekani kwa muda mfupi na mnamo mwaka 1993 mwishoni alirejea nyumbani na kushiriki harakati za siasa na kuwa Mbunge kwa takriban miaka 10 kuanzia 1995.

Kurejea kwa Dk Kabourou nchini na kujiunga na siasa kuliweza kuwa chachu kwa vijana si tu wa Kigoma bali nchini kote.

Kwa Kigoma Dk Kabourou atakumbukwa kwa jinsi alivyokuwa mvuto kwenye mikutano yake ama ya kampeni au ya kawaida. Mvuto huo uliwezesha akapewa jina RUKUGA ambao ni moja kati ya pepo kali zivumazo ndani ya Ziwa Tanganyika na ambazo wavuvi na wenye vyombo vya ussfiri majini huzigwaya sana.

Dk Kabourou atakunbukwa kwa kufufua mkusanyiko wa vijana waogeleaji kwenye mchezo maarufu wa AIFOLA.

Kumuelezea Ndugu Amani Walid Kabourou sio kwepesi kama inavyoweza kudhaniwa na kwa mimi ambae tunayo historia ya kipekee baina yetu.

Itoshe nihitimishe kwa yafuatayo kuwa binafsi nimesononeshwa kwakutopata wasaa wakushiriki mazishi yake,lakini hii imetokana na afya yangu kutokuwa nzuri.Hata hvyo. Nichukue fursa hii kumpa pole mjane pamoja na watoto wote wakiwemo Vyema,Walid Aman Walid Kabourou Jr na wengine wote. 

Aidha niwafariji ndugu jamaa na wote walioguswa na kuondoka kwa mpendwa wetu. Kikubwa tumuombee safari yake ya mwisho iwe nyepesi na ALLAH amsamehe makosa yake na kwa wana Kigoma tutafakari namna bora ya kumuenzi ndugu yetu. 

Wala tusiseme RUKUGA amepoa na kwamba amekuwa AIFOLA MWENDA SALAMA.

MZEE JOSEPH MUNGAI AFARIKI DUNIA, RAIS DKT. MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI

TANZIA:SPIKA WA ZAMANI WA BUNGE SAMWELI SITTA AFARIKI DUNIA,RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI

 SPIKA wa zamani wa Bunge la Tanzania, Samwel Sitta amefariki dunia usiku wa kuamkia leo nchini Ujerumani alikokua akipatiwa matibabu.

Rais John Magufuli tayari amemtumia salamu za pole Spika wa Bunge Job Ndugai na familia kufuatia msiba huo mzito.

Wanamuziki wajitokeza kwa wingi kumzika gwiji Kassim Mapili

 Mwanahabari nguli Hemedi Kimwanga (kushoto waliosimama) akipeana pole na wanamuziki mbalimbali wakongwe wakati wa msiba wa Mzee Kassim Mapili Magomeni Mapipa jijini Dar es salaam leo

 Wanamuziki nyota wa kike walijitokeza kwa wingi katika msiba huu. Hapo kuna Nyota Abdallah, Anna Mwaole, Kida Waziri, Lwiza Mbuttu, Asha Salvador na wengineo wengi
 Kanku Kelly na Papaa Juma Mbizo wakimuaga Kassim Mapili
Banana Zorro, Ben Kinyaia, Mrisho Mpoto na mdau wa muziki 
 Mzee Makassy na wakongwe wenzie walikuwepo
 Kanku Kelly na Delphine Munumba wakiongea na kaka Emmanuel Mpangala msibani
 Mwakilishi kutoka Wiziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo akitoa rambirambi za serikali 
 Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akimfariji mtoto wa marehemu
  Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akimfariji mtoto wa marehemu
  Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akimfariji mtoto wa marehemu
  Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akipeana mikono na mwanamuziki mkongwe Mjusi Semboja huku akiongea na Mzee Makassy na wanamuziki wengine
 Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akiongea na mchambuzi wa muziki wa dansi mahiri Zomboko na mdau wa muziki Hassan

MAZISHI YA DADA WA RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE KIJIJINI MSOGA

 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akimfariji mke wa Rais Mtaafu Mama Salma Kikwete alipowasili kuhudhuria mazishi ya Marehemu Tausi Khalfani Kikwete, dada wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015
 Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akimpokea Rais Mstafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi katika mazishi ya Marehemu Tausi Khalfani Kikwete, dada yake kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015
 Mbunge wa Chalinze Mhe Ridhiwani Kikwete akimlaki Rais Mstafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi alipohudhuria katika mazishi ya shangazi yake Marehemu Tausi Khalfani Kikwete, kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015
 Mama Salma Kikwete akipewa pole na Mama Sitti Mwinyi katika mazishi ya wifi  yake Marehemu Tausi Khalfani Kikwete, kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015
 Mama Salma Kikwete akipewa pole na Mama Khadija Mwinyi katika mazishi ya wifi  yake Marehemu Tausi Khalfani Kikwete, kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015
 Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akimpokea Mama Janet Magufuli katika mazishi ya  dada yake Marehemu Tausi Khalfani Kikwete, kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015
 Mama Salma Kikwete akimpoke Mama Janet Magufuli katika mazishi ya wifi  yake Marehemu Tausi Khalfani Kikwete, kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015
 Rais John Pombe Joseph Magufuli akipokewa na Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili kuhudhuria mazishi ya dada yake Marehemu Tausi Khalfani Kikwete kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015
  Rais John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi alipowasili kuhudhuria mazishi ya dada yake Mhe Kikwete Marehemu Tausi Khalfani Kikwete,  kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015. Kushoto ni Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Ghalib Bilal
  Rais John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally alipowasili kuhudhuria mazishi ya dada yake Mhe Kikwete  Marehemu Tausi Khalfani Kikwete, kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015
 Mama Janet Magufuli (kulia) akiwa na wafiwa kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015
 Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally akitoa hutba wakati wa mazishi 
 Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally akiongoza swala 
 Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa  mazishi ya dada yake Marehemu Tausi Khalfani Kikwete, kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21
 Rais Joseph Pombe Joseph Magufuli akiweka udongo kaburini
 Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiweka udongo kaburini
 Ni wakati wa dua baada ya mazishi
Rais Joseph Pombe Joseph Magufuli na Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete wakiondoka makaburini baada ya mazishi. PICHA NA IKULU