MBUNGE wa Korogwe Vijijini (CCM) mkoani Tanga, Steven Ngonyani maarufu Profesa Majimarefu amefariki dunia leo Jumatatu Julai 2, 2018 usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Taarifa za kifo cha mbunge huyo zimethibitishwa na ofisa uhusiano wa Muhimbili, Aminiel Eligaeshi.
Juni 20, 2018 Majimarefu alihamishiwa kwa ndege kutoka mkoani Dodoma kwenda MNH kwa matibabu huku ugonjwa uliokuwa ukimsumbua mbunge huyo haujawekwa wazi.
Juni 6, 2018 mbunge huyo alifiwa na mkewe, Mariam aliyekuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali hiyo hiyo ya Muhimbili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni