Watafiti
wa Kodi Barani Afrika wameshauriwa kuimarisha mtandao wao ili kuweza
kusaidiana kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili katika jitihada
zao za kufanya utafiti.
Ushauri
huo umetolewa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) Bw. Michael John wakati akifunga warsha ya
mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Mtandao wa Watafiti wa Kodi
Afrika (ATRN) ambayo imeandaliwa na Taasisi ya Usimamizi wa Kodi Barani
Afrika (ATAF) kwa kushirikiana na Chuo cha Kodi (ITA).
Bw.
Michael amesema kwamba watafiti hao wanategemewa sana na mamlaka za
mapato wanazoziwakilisha hivyo kuwataka kutumia ujuzi wa utafiti
walioupata wakati wa mafunzo hayo ya siku nne kutatua changamoto
mbalimbali na kuziongezea uwezo mamlaka za mapato barani Afrika hivyo
kupelekea kuongeza makusanyo.
“Nina
imani kwamba baada ya mafunzo haya mtaendelea kushirikiana kupitia
mtandao wenu ili kwa pamoja mtimize lengo lenu la kutatua changamoto
katika utekelezaji wa taratibu, sheria na sera za kodi barani Afrika
kupitia utafiti mtakaoufanya”.Aidha
amewataka watafiti hao kuzitumia vyema nyenzo za ukusanyaji na
uchambuzi wa taarifa ambazo wamepatiwa wakati wa mafunzo hayo ambayo
yamefanyika Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
huyo wa Rasilimali Watu na Utawala ameipongeza Taasisi ya Kodi Barani
Afrika pamoja na Chuo cha Kodi kwa kuandaa na kufanikisha mafunzo hayo
ambayo ni muhimu katika utendaji wa usimamizi wa Kodi barani Afrika.
Naye
Mkuu wa Chuo cha Kodi Pro. Isaya Jairo ameishukuru ATAF na TRA kwa
kukiamini Chuo cha Kodi kuendesha mafunzo kwa watafiti ambao wametoka
nchi mbalimbali za Afrika. Ambapo pia amewapongeza washiriki hao kwa
kupatiwa nafasi kushiriki mafunzo hayo akisema kwamba ushiriki wao
unadhihirisha utayari wa mamlaka za mapato barani Afrika kutatua
changamoto zilizopo kwa kuwa na watafiti wenye weledi na ujuzi.
Awali
akifungua mafunzo hayo, kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania, Kaimu Kamishna wa Walipakodi Wakubwa Bw. Alfred Mregi alisema
kwamba Usimamizi wa Kodi katika Afrika unakabiliwa na changamoto
mbalimbali ambazo watafiti wanategemewa kuzitatua ili taasisi
zinazosimamia mapato Afrika ziwe rafiki kwa walipakodi na hatimaye
kuongeza makusanyo ya mapato ya ndani.
“Tunawategemea
nyinyi kufanya utafiti wa mifumo ya kodi na kutoa suluhisho na
mapendekezo kwa watunga sera na wasimamizi wa kodi”, alisema Bw. Mregi.
Warsha
ya mafunzo kwa Mtandao wa Watafiti Afrika iliwashirikisha watafiti
kutoka baadhi ya nchi za Afrika ambao mapendekezo yao ya utafiti
yamekidhi vigezo kwa mujibu wa Taasisi ya Usimamizi wa Kodi Barani
Afrika ambayo inaratibu Mtandao wa Wasimamizi wa Kodi Afrika kwa lengo
la kuwajengea uwezo waafrika kufanya utafiti katika usimamizi, sheria na
sera za kodi na kuwaunganisha watafiti hao na wanataaluma.
Washiriki
wa warsha hii ambayo ni ya Tatu kufanyika, wameishukuru ATAF na Chuo
cha Kodi kwa kuendesha mafunzo hayo wakisema kwamba imewapa uelewa zaidi
wa kuendelea na utafiti wao.
Mafunzo
hayo ambayo yaliendeshwa kwa lugha tatu: Kireno, Kifaransa na
Kiingereza yaliwashirikisha washiriki 24 kutoka, Jamhuri ya Kidemokrasi
ya Kongo, Niger, Msumbiji, Zambia, Zimbabwe, Togo, Benin, Cape Verde,
Tunisia, Ivory Coast, Kenya na Tanzania.
Mkurugenzi
wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw.
Michael John akimkabidhi mshiriki kutoka Tunisia Bw. Jabali Belhanssen
cheti cha ushiriki wa mafunzo ya utafiti ambayo yafanyika jijini Dar es
Salaam kwa ushirikiano wa Taasisi ya Usimamizi wa Kodi Afrika (ATAF) na
Chuo cha Kodi (IAT). Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Kodi
(ITA) Prof. Isaya Jairo, Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma na Utafiti Dr. Lewis
Ishemoi na Mwakilishi ATAF Bw. Eugenio Bras.
Mkurugenzi
wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw.
Michael John (katikati) akifuatilia matukio wakati wa kufunga na
kukabidhi vyeti kwa washiriki wa warsha ya mafunzo kwa Mtandao wa
Watafiti wa Kodi Afrika (ATRN) ambayo imefanyika jijini Dar es salaam.
Wengina kutoka kushoto ni; Mkufunzi wa mafunzo hayo Prof. Nicaise Mede
kutoka Benin, Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo, Naibu Mkuu
wa Chuo cha Kodi Taaluma na Utafiti Dr. Lewis Ishemoi na Mwakilishi wa
Taasisi ya Utafiti Barani Afrika (ATAF) Bw. Eugenio Bras.
Baadhi
ya washiriki wa Warsha ya Mafunzo kwa Mtandao wa Watafiti wa Kodi
Afrika (ATRN) waliosimama wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa
Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw.
Michael John (aliyekaa katikati) baada ya kufunga mafunzo hayo. Wengine
kutoka kulia ni, Mwakilishi wa Taasisi ya Utafiti Barani Afrika (ATAF)
Bw. Eugenio Bras, Naibu Mkuu wa Chuo cha Kodi Taaluma na Utafiti Dr.
Lewis Ishemoi, Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo na Mkufunzi
wa mafunzo hayo Prof. Nicaise Mede kutoka Benin
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni