Rais Dkt. John Magufuli amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro kuhakikisha inapofika kesho (Aprili 8, 2018) awe ameshawaingiza askari Polisi walionguliwa nyumba zao hapo awali katika nyumba mpya ambazo zimezinduliwa hii leo.
Dkt. Magufuli ametoa agizo hilo leo (Aprili 7, 2018) wakati alipokuwa anazungumza muda mchache alipomaliza kuzindua nyumba za askari zilizojengwa mkoani Arusha na kusema anawapa pole kwa majanga yaliyotokea ya kuunguliwa moto, huku akiwapongeza wadau mbali mbali waliojitolea kwa mioyo yao katika ujenzi wa nyumba hizo.
"Nimepata mawazo ni kitu gani tunaweza kufanya kuhusina na matatizo ya nyumba za Polisi, sasa ninachoomba Mhe. IGP wale walionguliwa nyumba, kesho waingie katika nyumba zao hizi mpya ambazo zimemalizwa kujengwa. Kwasababu najua muda mwingine wanaweza wakachomekwa Polisi wengine halafu waliokuwemo wakaambiwa hapana", amesema Dkt. Magufuli.
Pamoja na hayo, Rais Magufulia ameendelea kwa kusema "sasa nataka wale wale walionguliwa ndio waingie humo kwenye nyumba kwasababu Mungu aliwasaidia, moto ukaungua ungua kwa faida ya wao lakini hii inadhihirisha ni kwa namnagani makazi ya nyumba za polisi yalivyo kuwa mabovu"..
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni