Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) imesema kuwa kutua kwa Ndege kubwa ya ‘gorofa’ A380 ya Fly Emirates imedhihirisha kuwa uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Mwalimu Julius K Nyerere na vyombo vyake kuwa madhubuti katika usafiri wa anga.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Hamza Johari amesema kuwa ndege hiyo licha kupata udhuru wa kushindwa kutua katika uwanja wa ndege wa Mauritius kumeipa heshima nchi katika kuwa na viwango katika utaoaji huduma ya usafiri wa anga.
Amesema kuwa Rubani wa ndege A380 ya Fly Emirates alifanya busara ya kuamua baada ya kuona hali ya hewa ya Mauritius kutokuwa nzuri na kuamua kutua kwenye Uwanja wetu wa kimataifa wa Mwalimu Julius K Nyerere na kuamini kuwa atatua bila wasiwasi.
Johari amesema kufuatia kutua kwa ndege hiyo kubwa nchi imeweza kupata mapato katika huduma mbalimbali za kijamii kutokana na abiria waliokuwa katika ndege hiyo zaidi ya watu 500 ambao wote walilala katika hoteli zilizopo nchini.
Amesema kuwa ndege hiyo kubwa ya abiria duniani ndio mara ya kwanza kutua katika uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius K. Nyerere hivyo inaonyesha kujizatiti katika utoaji katika utoaji wa huduma ya usafiri wa anga.
Ndege hiyo imetua Aprili 24 katika uwanja wa Ndege Mwalimu Julius Nyerere ikitokea Dubai ambaye ilishindwa kutua mara tatu katika uwanja wa Mauritius na kuja kutua Tanzania
Mkurugenzi Mkuu huyo amesema kuwa wamekuwa na asilimia 64 kutoka 37 kwa viwango vilivyowekwa na Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) hivyo tuzo yake itatolewa na Rais wa shirika hilo kwa kumkabidhi Rais Dk.John Pombe Magufuli na mawasilino yanafanyika yanafanyika ujio wa Rais wa ICAO.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari akizungumza na waandishi habari kuhusiana na kutua kwa ndege kubwa ya ya Emirate abiria duniani ya A380 ya Ghorofa iliyotua katika uwanja wa Ndege wa Mwalumu Julius Nyerere , jijini Dar es Salaam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni