Waziri
wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mhagama akizungumza na baadhi ya washiriki wa maonesho wakati wa
maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani Aprili
28, 2018 iliyoadhimishwa Kitaifa Mkoani Iringa.
Waziri
wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mhagama akiwasili katika Viwanja vya Kichangani Mkoani Iringa
wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani
Aprili 28, 2018.
Waziri
wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mhagama akitia saini katika kitabu cha wageni alipotembelea
banda la maonesho la OSHA wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na
Usalama Mahali Pa Kazi Duniani Aprili 28, 2018 Iringa.
Waziri
wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mhagama akiangalia mfano wa namna bora ya kumuokoa mfanyakazi
pindi apatapo ajari sehemu ya kazi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya
na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani Aprili 28, 2018 Iringa.
Waziri
wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mhagama akizungumza na Mzee Juma Nyinge aliyetembelea katika
mabanda ya maonesho wakati wa Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi
Duniani Aprili 28, 2018.
Afisa
Mahusiano na jamii kutoka Kampuni ya Acacia Bi. Agripina Joseph akitoa
maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu
wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea banda lao wakati wa
maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani.
Waziri
wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mhagama akiuliza swali kwa Afisa Usalama kazini Bw. Mlewa
Mustapha kutoka Mgodi wa Buzwagi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya
na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani.
Waziri
wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mhagama akipokea zawadi kutoka kwa Kampuni ya Acacia
waliposhiriki katika maonesho ya kuadhimisha Siku ya Afya na Usalama
Mahali Pa Kazi Duniani mkoani Iringa.
Mwalimu
wa wasioona Steven Changalo akiandika jina la mhe.Waziri Mhagama kwa
kutumia vifaa wezeshi alipotembelea banda la Chama cha Walimu Tanzania
(CWT) katika maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi
Duniani mkoani Iringa.
Waziri
wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mhagama akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw.Erick
Shitindi anayeshungulikia Kazi,Ajira, Vijana na wenye ulemavu.
Kaimu
Mtendaji Mkuu OSHA Bi.Khadija Mwenda akizungumza jambo wakati wa Kilele
cha Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani yaliyoadhimishwa
mkoani Iringa.
Katibu
Mkuu wa Ofisi hiyo Bw.Erick Shitindi anayeshungulikia Kazi,Ajira,
Vijana na wenye ulemavu akitoa salamu kwa washiriki wa Maadhimisho ya
Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani yaliyofanyika mkoani
Iringa.
Waziri
wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mhagama akitoa vyeti kwa washindi wa maonesho ya Siku ya Afya na
Usalama Mahali Pa Kazi Duniani yaliyofanyika mkoani Iringa.
Waziri
wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mhagama akihutubia wananchi na washiriki waliohudhuria wakati
Maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani
yaliyofanyika mkoani Iringa.
Waziri
wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mhagama (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na
wafanyakazi wa OSHA pamoja na watendaji wa Idara ya Kazi, Ajira, Vijana
na Wenye Ulemavu wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali
Pa Kazi Duniani yaliyofanyika mkoani Iringa. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
Serikali
imedhamiria kuendelea kukomesha ajira hatarishi za watoto ili
kuhakikisha kuwa watoto wanalindwa na kuwapa nafasi stahiki kulingana na
sheria na kanuni zilizopo nchini.
Hayo
yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu
wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipohudhuria katika kilele cha Siku
ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani inayoadhimishwa kila mwaka
tarehe 28 Aprili ambapo Kitaifa ilifanyika Mkoani Iringa.
Waziri
alieleza kuwa, katika mapambano haya ya ajira hatarishi kwa watoto ni
moja ya utekelezaji wa kampeni zinazolenga kuharakisha utekeleezaji wa
vipaumbele vilivyomo kwenye lengo namba (8) la Maendeleo Endelevu ya
Umoja wa Mataifa ambalo ni kuboresha mazingira ya wafanyakazi na
kukomesha ajira mbaya kwa watoto.
“Tuendelee
kupiga vita ajira mbaya kwa watoto kwa kuzingatia kampeni zilizopo hasa
ile ya kuboresha mazingira ya wafanyakazi ifikapo mwaka 2030 pamoja na
kukomesha ajira mbaya za watoto ifikapo mwaka 2025,” alisema Waziri
Waziri
aliongezea kuwa katika kuhakikisha watoto wanakuwa na mazingira salama ,
Lazima kuwe na mikakati ya pamoja baina ya utatu katika masuala ya kazi
na ajira ikiwemo na kujenga utamaduni wa kujikinga na vihatarishi
sehemu za kazi vinavyoweza kusababisha kuhatarisha afya na usalama wa
wafanyakazi.
Aidha
kama Taifa lazima tuoneshe umuhimu wa kuhakikisha kampeni hii inakuwa na
matokeo chanya na kuendelea kuwa na Taifa lenye maendeleo.
Waziri
aliongezea kuwa kulingana na Matokeo ya Utafiti wa Mtakwimu Mkuu wa
Serikali uliofanyika mwaka 2014 na matokeo yake kuchapishwa mwaka 2016
ulibainisha kuwa, hali ya ajira hatarishi za watoto kuzidi kuwa mbaya
zaidi katika sehemu za mashambani, sekta ya madini, misitu na uvuvi.
“Kwa
mujibu wa taarifa za Mtakwimu Mkuu wa Serikali za mwaka 2014 zilibaini
kuwa watoto wenye umri kati ya miaka 5-17 walioko kwenye ajira ni
takribani milioni 4.2 ambayo ni asilimia 28.8 ya wafanyakazi wote na
kati ya hao asilimia 21.5 wako kwenye ajira hatarishi hususan sehemu za
mashambani ambako asilimia 35.6 ya wafanyakazi wote ni
watoto”,alisisitiza Mhe.Waziri
Kwa
upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda alieleza kuwa
wataendelea kutekeleza majukumu yao kwa kuhakikisha sheria zilizopo
zinafuatwa bila kukiukwa hususan kwa makundi maalum iliwemo yale ya
vijana na makundi ya watu wenye ulemavu.
“kwa
kuwa Vijana wadogo ndiyo nguvu kazi ya taifa hivyo wanastahiri kulindwa
na kuangaliwa kwa jicho la pekee ili kuwa na kizazi endelevu,”alisema
Mwenda
AWALI
Aprili
28 ya kila mwaka ni siku ya Kimataifa ya kuadhimisha masuala ya Afya na
Usalama Mahali Pa Kazi, ambapo huwa na Kauli Mbiu inayotumika duniani
kote ambayo inatolewa na Shirika la Kazi la Duniani.Kauli mbiu ya mwaka
huu ni “Kizazi Salama chenye Afya – Generation Safe and
Health”.Kaulimbiu hiyo ili kuendana na mazingira ya nchi yetu
iliboreshwa na kuwa “Kizazi Salama Chenye Afya kwa Uchumi wa Viwanda
–Generation Safe and Health for Industrial Economy”.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni