Rais wa zamani wa Botswana, Sir Ketumile Masire amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 91.
Taarifa zilizotolewa zinasema Sir Masire alifariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa hospitali alikokuwa amelazwa toka wiki iliyopita.
Sir Ketumile Masire alikuwa Rais wa Botswana kuanzia mwaka 1980 hadi 1998 na enzi za uhai wake aliongoza juhudi mbalimbali Barani Afrika ikiwa ni pamoja kuongoza tume iliyochunguza mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni