MJAMZITO SERENA WILLIAMS AJIANIKA UTUPU KATIKA JARIDA LA VANITY FAIR

Mjamzito Serena Williams amepiga picha akiwa utupu itakayotumika katika ukurasa wa mbele wa jarida la Vanity Fair.

Nyota huyo wa tenesi alibaini kuwa ni mjamzito akitarajia kupata mtoto wake wa kwanza na muasisi wa Reddit, Alexis Ohanian kabla ya michuano ya Australian Open, Januari.

Serena ameliambia jarida la Vanity Fair kuwa alikuwa hajahisi jambo lolote kuhusu ujauzito wake hadi pale alipojisikia kuugua akiwa uwanjani akifanya mazoezi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni