Mahakama ya Kuu ya Venezuela
imeshambuliwa kwa mabomu yaliyodondoshwa na helkopta katika kile
rais wa nchi hiyo Nicolás Maduro alichokiita kuwa ni shambulizi la
kigaidi.
Picha zilizowekwa kwenye mitandao ya
kijamii zinaonyesha helkopta ya polisi ikizunguka angani kabla ya
kuachia mabomu na kusikika mlipuko mkubwa, kitendo kilichofanywa
na polisi.
Afisa wa polisi anayesemekana kuiba
helkopta hiyo, alitoa taarifa akiishutumu serikali kwa kuiita kuwa ni
ya kihalifu. Rais Maduro amekuwa akikabiliwa na maandamano ya umma.
Polisi wa Venezuela wakiwa wamelizingira jengo la Mahakama Kuu baada ya kulipuliwa mabomu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni