Waislamu waliokuwa bado wapo macho wakingojea kula daku katika jengo la ghorofa lililoungua moto Jijini Lindon wamepongezwa kuwa mashujaa baada ya kuwaokoa majirani zao kwa kuwaamsha.
Wakazi Waislamu wa jengo hilo la Grenfell Tower, walikuwa macho katika mwezi huu wa mfungo wa Ramadhani wakingojea kula daku walianza kusikia harufu ya moshi na kisha kuona moto majira ya saa saba usiku.
Baada ya kuona hali hiyo walihaha kukimbia kwenye milango ya majirani zao waliokuwa wamelala na kugonga milango yao kuwaamsha, kutokana na jengo hilo kutokuwa na alamu ya moto wala mifumo ya maji ya kuzimia moto.
Baadhi ya wakazi wa jengo hilo ambao ni waumini wa dini ya Kiislamu wakiwa mita kadhaa kutoka jengo linaloungua
Mama huyu mkazi wa jengo la ghorofa la Grenfell Tower lililoungua akiangua kilio
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni