Watu sita wameuwawa na wengine wapatao 48 kujeruhiwa katika shambulizi la kigaidi Jijini London ambapo washambuliaji watatu wanaume nao wameuwawa kwa kupigwa risasi na polisi.
Gari jeupe liliwagonga watembea kwa miguu katika daraja la London jumamosi na kisha watu watatu wakatoka kwenye gari hilo na kuwachoma visu watu kadhaa katika soko Borough lililopo karibu na daraja hilo.
Mmoja wa majeruhi akiwa amebebwa kwenye kitanda chenye magurudumu akiwahishwa katika gari la wagonjwa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni