WATUMISHI KATIKA HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO IPASAVYO

Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha Ernest Mpanda akiwa anazungumza katika kikao cha kuimarisha Utendaji  katika Halmashari ya Jiji ,aliyepo kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro ,aliyepo kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Juma Kihamia 
 
 Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro akizungumza na Watumishi wa Halamashauri ya Jiji la Arusha katika kikao hicho kilichofanyika leo 
 
 Baadhi ya watumishi waliobhudhuria katika kikao hicho kilichofanyika leo.


Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro akiwa anasisitiza jambo katika kikao hicho kilichofanyika katika leo Jijini Arusha.
Katubu wa CCM mkoa wa Arusha Ernest Mpanda akisistiza jambo katika kikao kilichofanyia cha watumishi katika Halmashauri ya Jiji la Arusha



 Kikao kinaendelea baadhi ya watumishi wakiwa wanafuatilia yanayoendelea Picha na Mahmoud Ahmad


Na, Mwandishi wetu Arusha.

Katibu wa CCM mkoa wa Arusha Ernest Mpanda amekutana na watumishi katika Halmashauri ya Jiji  la Arusha ambapo amesema kuwa serikali ya awamu ya tano inatambua na kuthamini kazi kubwa wanayoifanya ,huku chama hicho kikiwa na imani ya kwamba binadamu wote nisawa,heshima ,kutambuliwa pamoja na Ujamaa na kujitegemea.


Ameyasema haya leo katika kikao cha kuimarisha utendaji kazi na  kuwataka watumishi hao kuutanguliza Uzalendo mbele,wafanye kazi kwa manufaa ya Taifa na kwa Watanzania kwa ujumla , kwa maadili na kwa usahihi.

"wakati wa kupiga umekwisha,hatutakubali tumekupa uongozi  hukuwa na mali nyingi, ndani ya miaka miwili  unakutwa unazo mali nyingi ulizojilimbikizia bila kufahamika vyanzo vyake lazima tutakuhoji,kila mtu atimize wajibu wake kwa kumuogopa Mungu" alisema katibu huyo.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro amesema kuwa ni vyema kila mtumishi akasimamia eneo lake la kazi ipasavyo bila kuingiza undugu kwenye kazi,kwani kila mmoja akisimamia eneo lake kikamilifu hakuna mtu yeyote yule atakayekuwa na shida na wao.

"Umepewa eneo lako la uitumishi lisimamie ipasavyo usilete undugu kwenye kazi,ukifanya kazi yako vizuri hakuna mwenye shida na wewe,unalipwa mshahara ni vyema ukajiuliza je unafanya kazi kama ipasavyo?"alihoji mkuu wa wilaya .

Aidha Daqqaro amewataka watumishi hao kuwahudumia wananchi kwa moyo safi,lugha nzuri ,kila mmoja afanye kazi yake kwa usahihi japokuwa wananchi wengine wanakera ,amewataka kutambua kuwa mwisho wa siku wao ndiyo wameajiriwa na siyo wale ambao wanawahudumia. 

"Wahudumieni kwa moyo safi na lugha nzuri,tendeni kazi kwa kuzingatia maadili na kwa usahihi,usije ukapigiwa simu na kiongozi wako ukaanza kuingiwa na hofu na kujiuliza kuna jambo gani tena" alisisitiza Daqqaro.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni