CHAMA CHA WAONGOZA WATALII TANZANIA (TTGA) WALIA NA MIUNDO MBINU MIBAYA YA BARABARA NDANI YA HIFADHI ,WASEMA HADI SASA MIKATABA IMEKUWA DONDA NDUGU KWAO!

Wa pili kulia ni mwenyekiti wa Chama cha  waongoza Utalii Nchinni Tanzania Halifa Msangi,Wa kwanza kushoto Katibu wa chma hicho Emanuel Mollel,wakiwa na wajumbe wa chama hicho ,pamoja na Hosiana F. Siao
Wakizungumza na wageni mbalimbali Ambao walitembelea banda lao katika maonyesho ya Utalii yaliyo shirikisha zaidi ya makampuni  300 ya utalii,amabapo washiriki wa ndani yanchi ni 60% na yale ya nje ni 40% ambapo huwa wanafanyika lila mwishoni mwa mwezi mei .
Chama cha waongoza Watalii wakiwa kwenye banda lao ndani ya viwanja vya magereza katika maonyesho ya Karibu Fair yaliyo beba kauli mbiu isemayao Utalii endelevu kwa Maendeleo.
Maongezi yakiendelea na wageni waliotembelea banda lao.Picha na Mahmoud Ahmad


Chama cha waongoza Watalii nchini Tanzania (TTGA) wameiomba Serikali iwapatie eneo huru kati ya Hifadhi  ya Ngorongoro na ile ya  Serengeti ,kwani katika eneo hilo la Ndutu katika upande wa Serengeti hakuna barabara za kufanyia mizunguko za kwenda kuangalia wanyama .

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa chama hicho ndugu Halifa Msangi  kwamba  changamoto kubwa wanayoipata kama waongoza watalii ,ni kipindi ambacho wanyama pundamilia na Nyumbu wanapohama  kuelekea upande mwingine hawawezi kuwapeleka wageni kwenda kuwaona wanyama hao upande wa pili

"Katika eneo la Ndutu wananyama pundamilia na nyumbu huwa wanatabia ya kuhama na kuelemea  upande mwingine,sasa unakuta wewe muongozaji ukiwa na kibali cha upande mmoja tu  huwezi kuwapeleke wageni mahali wanyama walipo kwani hakuna barabara ya kufanyia mizunguko kwenda kuwaona wanyama jambo ambalo tumekuwa tukipata changamoto kubwa na maswali mengi kutoka kwa wageni tumeizungumzia changamoto hii kwa muda mrefu sasa."alisema Halifa.

Kwa upande wake Katibu wa chama hicho cha waongoza watalii Emanuel Alfayo Mollel amesema kuwa changamoto nyingine kubwa ni barabara zilizopo ndani ya Hifadhi haswa kutoka Ngorongoro kuelekea Serengeti ,barabara hizo zimejazwa vifusi kwa ya km 10 ambavyo havijasambazwa jambo ambalo wakati mwingine vinaweza vikapelekea hata kusababisha ajali pale ambapo dereva anahangaika kuvikwepa.

''jamani miundo mbinu ndani ya hifadhi  haswa  Tarangire na Manyara ni changamoto kubwa wakati wa mvua hakupitiki, "alisema Emanuel.

Amesema kuwa asilimia 90 ya waongoza Watalii ni waajiriwa kwenye makampuni ya Utalii ,hadi sasa mikataba yao imekuwa ni donda ndugu kwani mikataba hiyi ipo tayari lakini hakuna wakuisimamia ili ifanye kazi kama inavyohitajika.

Amesema  Waongoza watalii nchini Tanzania kilianzishwa mwaka 1999,kina jumla ya wanachama zaidi ya 3000 ,Wanachama ni 1130 ,wanachama hai waliolipa ada zao kwa mwaka 2017 ni 567 tu,amewataka waongozaji watalii hao ambao sio wanachama waamue kuiunga kwani hakuna njia nyingine ya kutatua changamoto waliyonayo zaidi ya kuwa wamoja.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni