UKWELI KUHUSU MTI ULIOGOMA KUNG'OLEWA JIJINI MWANZA.


                                                                                         George Binagi-GB Pazzo @BMG
 

Wakazi wa Jiji la Mwanza wameingia katika taharuki baada ya kutokea uvumi wa taarifa za mti kugoma kung’olewa katika eneo la Pasiansi ambapo kuna shughuli ya upanuzi wa barabara inayoelekea uwanja wa ndege wa Mwanza.

Taharuki hiyo ilianza tangu jana majira ya jioni ambapo mamia ya wananchi walijazana katika eneo hilo ili kushuhudia mgomo wa mti huo ambao inasadikika ulikuwa ukitoa sauti za kulalama mithiri ya binadamu.

Zoezi la kuung’oa mti huo aina ya mwembe limefanikiwa hii leo majira ya saa tatu asubuhi baada ya shughuli pevu ya kuung’oa kwa kutumia mashine aina ya burudoza huku baadhi wakihusisha tukio hilo na imani za kishirikina na wengine wakisema ni upotoshaji tu ulifanyika juu ya tukio hilo.

Kasim Mlisu ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya ujenzi ya Nyanza Road Works inayojenga barabara ya Pasiansi, amesema taarifa za mti huo kuzungumza ni za upotoshaji na kwamba zoezi la kuung’oa lilichukua muda mrefu tangu juzi ili kupisha hatua za upimaji wa ukubwa wake na kusubiri mashine aina ya“skaveta” iliyofanikiwa kuung’oa.

Katibu wa Chama cha Tiba asilia mkoani Mwanza CHAWATIATA, Kawawa Athuman, amesema tukio la mti kuzungumza ama kugoma kung’olewa halina ukweli wowote kwa karne hii ya 21 japo matukio ya aina hiyo yalikuwepo enzi za kale kabla ya ujio wa dini barani Afrika ambapo amewatahadharisha watumiaji wa mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kujiepusha na usambazaji wa taarifa za upotoshaji.


Zoezi la kuung'oa mti likiendelea
Hapa msumeno ulikata ila mti ukagoma kuangua licha ya kuvutwa
Zoezi la kuung'oa mti huo likiwa limefanikiwa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni