Shule ya msingi Sing’isi iliyopo katika wilaya ya Arumeru Mkoani
Arusha iliyokuwa ikikabiliwa na changamoto ya madarasa kujaa maji
imepatiwa msaada wa kiasi cha shilingi Milioni nne na benki ya biashara
ya Africa (CBA) kwa ajili ya ukarabati wa baadhi ya madarasa
Akikabidhi
hundi katika shule hiyo juzi Mkurugenzi wa CBA Gifti Shoko alisema kuwa
lengo la msaada huo ni kusaidia wanafunzi kuondokana na changamoto ya
kutoa maji katika madarasa pindi mvua zinaponyesha hali inayosababisha
kukosa vipindi viwili hadi vitatu kwa siku
Alisema
kuwa msaada huo utumike kama ulivyokusudiwa kuboresha madarasa hayo
kwani ubora wa elimu unaletwa na mazingira mazuri ya watoto kusomea
‘’Hapa
nawaona Marais, mawaziri wa kesho pamoja na wafanyakazi wazuri wa benki
yetu hivyo hatuna budi kutuoa msaada huu ikiwa kama mchango wetu wa
kuboresha sekta ya elimu na tunawahidi hatutaishia hapa tutaendelea
kuwasaidia kadri ya uwezo wetu ‘’
Mwalimu
mkuu wa shule hiyo Faith Mushiro akitoa neno la shukrani alisema kuwa
wanafunzi wa darasa la tano na la sita ndiyo hasa walikuwa wakipata
hadha hiyo ya kuondoa maji madarasani pindi mvua zinapoanza kunyesha
Aidha
alisema kuwa zaidi ya vipindi viwili hadi vitatu vya asubuhi hushindwa
kuhudhulia kutokana na changamoto hiyo hivyo kupitia msaada huo
wanafunzi watasoma katika vyumba vya madarasa vizuri tofauti na kipindi
cha nyuma
Awali
akisoma Risala mwalimu wa shule hiyo Bw.Simon Mbawala kwa niaba ya
shule hiyo alisema kuwa pamoja na msaada waliopatiwa bado shule
inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa makataba ya kuhifadhi vitabu,
kuharibika kwa sakafu za madarasa pamoja na kupasuka kwa vioo vya
madirisha
Hata
hivyo tunatoa shukrani zetu za dhati kwa mssada huu wa ujenzi wa vyumba
vinne ambayo vilikuwa na tatizo la kuvuja kwa maji kutokana na bati
zake kuwa chakavu hali iliyokuwa ikiwathiri sana wanafunzi na walimu
hasa ikifika wakati wa kufundisha
Mkurugenzi
wa Benki ya biashara ya Africa (CBA) Gifti Shoko akikabidhi hundi ya
kiasi cha shilingi Milioni nne kwa Mwalimu mkuu wa Shule ya msingi
Sing’isi iliyopo katika wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha juzi Bi.Faith
Mushiro kwaajili ya kukarabati madarasa manne ambayo hujaa maji kipindi
cha mvua hali ambayoilikuwa ikiwasababishia wanafunzi kukosa vipindi
viwili hadi vitatu kwa siku.
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi Sing'isi Bi.Faith Mushiro akionyesha sehemu
ambayo husababisha maji kujaa ndani ya madarasa pindi mvua inaponyesha,
wakatikati ni Mkurugenzi wa Benki ya biashara ya Africa(CBA)Gifti Shoko
pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo
Mwalimu
Mkuu wa shule ya msingi Sing'isi Bi.Faith Mushiro akitoa neno la
shukrani kwa uongozi wa benki ya CBA mara baada ya kupata msaada wa
shilingi Millioni nne kwa ajili ya ukarabati wa madarasa.
Mkurugenzi
wa Benki ya biashara ya Africa(CBA)Gifti Shoko akiangalia baadhi ya
vifaa vya umeme ambavyo walitoa msaada kwa shule hiyo
Wanafunzi wakiimba
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni