Msemaji wa rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amesema rais huyo huwa halali katika mikutano kama inavyodaiwa bali hufumba macho yake kwa muda mrefu ilikuyapumzisha.
Msemaji huyo George Charamba amesema rais Mugabe hufumba macho kuyaepusha na mwanga.
Imekuwa kawaida sasa kwa rais Mugabe kulala kwenye matukio kadhaa na kuibua hofu ya hali ya afya yake.
Rais Mugabe hivi karibuni amekuwa akipatiwa matibabu maalum ya macho nchini Singapore.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni