Vyombo vya habari nchini Kenya
vitaendesha midahalo mitatu ya wagombea urais mwezi mmoja kabla ya
Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Agosti mwaka huu.
Midahalo hiyo ya urais itafanyika
katika tarehe tofauti mwezi Julai, huku mdahalo wa kwanza wa marais
ukipangwa kufanyika Julai 10.
Mdahalo wa wagombea mwenza utafuatia
Julai 17 na kisha mdahalo wa mwisho wa wagombea urais Kenya kufanyika
Julai 24.
Midahalo hiyo yote itafanyika kwenye
chuo cha Catholic University of Eastern Africa saa moja na nusu usiku
na kurushwa kwenye runinga na redioni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni