NAIBU MKURUGENZI WA IMF AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI


Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Amina Khamis Shaabani (kushoto) wakijadili jambo kabla ya kuwasili kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustino Mahiga, muda mfupi kabla ya kuwasili kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Katikati ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb).
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto), akisikiliza jambo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakirisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba (kulia) katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere muda mfupi kabla ya kuwasili kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (kulia) wakifurahia jambo baada ya kusoma habari kuhusu ujio wa Zhang hapa nchini ambapo alikiri kutoa taarifa na kusudi la ujio wake zilizoandikwa na Gazeti la Daily News. Ni muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni