Mmoja ya waratibu elimu kata Salumu Myeka wakifuatilia kwa makini wakiwa na wadau wenzake shughuli nzima ya utoaji wa zawadi
Na Mahmoud
Ahmad Kondoa
Mkuu wa
wilaya ya Kondoa Sezaria Makota amewataka waalimu,watendaji na wadau wa elimu wilayani humo kuhakikisha ufaulu wa
wanafunzi unavuka lengo walilojiwekea sanjari na kuhakikisha maabara
zinakamilika kwa wakati kwenye shule mbalimbali ili vifaa vya maabara walivyoahidiwa
na wizara ya elimu wapewe kwa wakati.
Kauli hiyo
ameitoa kwenye sherehe za tathmini ya sekta ya elimu wilayani humo iliyofanyika
kwenye ukumbi wa Kondoa Irangi wilayani humo.
Amesisitiza
kuwa suala la kuwapati elimu watoto wilayani humo ni jukumu ambalo linahitaji
ushirikiano wa wadau wote wa elimu wilayani humo na si suala la walimu pekee
hivyo kwa umoja wao wanatakiwa kutoa ushirikiano ili kuweza kufanikiwa kufikia
malengo katika sekta hiyo.
“Tumekuwa
nyuma katika sekta ya elimu hivyo nawasihi wadau wote kuhakikisha wanafunzi
wilayani hapa wanapata huduma muhimu ilikuweza kufikia malengo tarajiwa ya
ufaulu wao na kuweza kuwa kwenye kumi bora za shule bora hapa nchini naahidi
kulivalia njuga suala hilo ilikuweza kufikia malengo”alisisitiza Dc Makota.
Kwa Upande
wake mkurugenzi wa wilaya Kondoa Vijijini Falessy Kibassa alisema kuwa
atahakikisha kuwa suala hilo linafanikiwa lengo likiwa kuwawezesha waalimu na
wadau kufikia malengo tarajiwa ya ufaulu na atalivalia njuga katika kuhakikisha
masuala ya elimu wilayani humo yanakuwa ya mafanikio na mfano wa kuigwa mkoani
hapa.
“Nasisitiza
kutoa ushirikiano kwa wadau wa elimu na waalimu wilaya kwangu na milango ipo
wazi kwa wadau kutoa maoni pale wanapoona kunalega katika sekta hii”alisisitiza
Kibasa
Nae Afisa elimu
msingi Alphonce Mwamwile alisema kuwa sekta ya elimu wilayani humo japokuwa inakabiliwa
na changamoto kubwa za uhaba wa waalimu katika shule nyingi wilayani hapa
pamoja na utoro,ukosefu wa chakula mashuleni wakati wa mchana watajitahidi
kuhakikisha elimu inakuwa sanjari na ufaulu wa wanafunzi.
Afisa elimu
Sekondari Hildacard Saganda alisema kuwa
kumekuwepo na changamoto kubwa ya umaliziaji wa maabara katika shule za
sekondari hivyo kuwakosesha wanafunzi wanaojifunza masomo ya sayansi kukosa
kujifunza kwa vitendo ila watahakikisha wanashirikiana na wadau wengine katika
kutatua changamoto hiyo.
Kwa upande
mwingine Mbunge wa Kondoa vijijini Ambaye pia ni naibu waziri wa Fedha na
Mipango Ashatul Kijaji ameahidi kutoa Photocopy mashine kwa ajili ya mitihani
ya kila mwezi kwa wanafunzi wa shule za wilaya hiyo
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni