MBUNGE PANGANI AWATAKA WANANCHI KUWEKEZA KWENYE KILIMO ILI KUPATA MAFANIKIO

MBUNGE wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso amewataka wananchi kuwekeza kwenye kilimo chenye tija kwa kuongeza uzalishaji ili waweze kupata mafanikio na kijikwamua kichumi.

Aweso aliyasema hayo wakati akizungumza na Mtandao huu ambapo alisema
wilaya ya Pangani imejaliwa kuwepo na ardhi yenye rutuba ambayo inaweza
kustawisha mazao ya aina yoyote.

Alisema kutoka na fursa hivyo wananchi wanapaswa kuitumia kama mtaji wa
kuweza kulima kilimo chenye manufaa ambacho kinaweza kuwa mkombozi
wao.

Aidha pia alisema lazima wabadilike waona namna ya kuchangamkia fursa
mbalimbali zilizopo ikiwemo mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kwa
kuongeza wigo mpana wa kujikita kwenye kilimo.

“Mradi mkubwa wa bomba la mafuta hii ni fursa kubwa hivyo lazima
wananchi wa Jimbo langu la Pangani waone ni vipi wanaweza kuitumia kwa
kuongeza uzalishaji wenye tija na manufaa kwao “Alisema.

Hata hivyo aliwataka wakazi wa wilaya hiyo kushikamana kwa pamoja ili
kuweza kupata maendeleo ikiwemo kuongeza bidii katika kuzalisha mazao
mbalimbali yanayolimwa na kustawi vizuri.

Hata hivyo aliwataka kulinda maeneo yao na kuacha kuyauza jambo ambalo
linaweza kuwarudisha nyuma kimaendeleo na kujikita wakishindwa kuendana
na ujio wa fursa mbalimbali ikiwemo mradi wa bomba la mafuta.

“Ndugu zangu wananchi wanaweza kutokea watu wakawarubuni muwauzie maeneo yenu niwaambie tu achane kuuza maeneo yenu ovyo kutokana na ujio wa fursa hiyo muhimu “Alisema.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni