Askofu Dedmond Tutu wa Afrika Kusini amebainisha kuwa anataka kuwa na fursa ya kuomba kusaidiwa kufa.
Mshindi huyo wa tuzo ya Nobel na mwanaharakati wa kupinga ubaguzi, amesema hataki kulazimishwa kuendelea kuishi kwa gharama zozote.
Matamshi hayo ya Tutu yameandikwa na yeye katika gazeti la Washghton Post wakati akitimiza miaka 85 ya kuzaliwa.
Mnamo mwaka 2014 Askofu Tutu alibainisha kuwa anaunga mkono wagonjwa mahututi kusaidiwa kufa, lakini alikuwa hajaeleza iwapo yeye pia angependa kusaidiwa kufa.
Mwezi uliopita Askofu Tutu alikuwa amelazwa na kufanyiwa upasuaji ili kumtibu maambukizi ambayo yamekuwa yakijirudia rudia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni