Waziri
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza na
wakuu wa Taasisi na Idara za wizara (hawapo pichani), wakati wa kikao
cha kujadili masuala mbalimbali ya mipango na maendeleo ya wizara.
Kulia ni Naibu Waziri Mhandisi Hamad Masauni. Kikao hicho kimefanyika
leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu, akizungumza wakati wa
kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya mipango na maendeleo ya
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Idara zake. Kikao hicho kiliongozwa
na Waziri wa wizara hiyo, Mwigulu Nchemba (hayupo pichani). Kushoto ni
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Minja. Kikao hicho
kimefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, jijini Dar es
Salaam.
(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni