MKUUWA WILAYA YA ILALA AFANYA ZIARA YA KUPAMBANA NA KERO ZA WANANCHI PUGU NA GONGOLAMBOTO, DAR ES SALAAM
posted on
Mkuu wa wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, Sophia Mjema akisaini kitabu cha wageni alipowasili kufanya mkutano wa hadhara wakupambana na kero za wananchi katika Uwanja wa Soko la Kigogo Fresh, Pugu, wilayani humo,jana. Kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ambaye aliambatana na mkuu huyo wa wilaya katika ziara hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akimsikiliza kwa makini Katibu Tawala wa Kata ya Ukonga, Jeremia Makorere kabla ya mkutano huo. Katikati ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edwardmpogolo
Mbunge wa Ukonga Ndugu Waitara akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema wakati akielekezwa jambo wakati wa mkutano huo wa Pugu
"Lazima tusaidie wananchi hawa bila kujalai itikati za vyama vyetu vya siasa", Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akimsisitizia, Mbunge wa Ukonga Ndugu Waitara wakati wa mkutano wa kutatua kero za wananchi katika Soko la Kigogo Fresh, Pugu, Wilayani humo
Diwani wa Kata ya Pugu, Boniventure Mphuru akimsalimia Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema alipowasili kwenye mkutano huo. Kushoto ni Waitara na Watatu Kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edrwad Mpogolo
Katibu Tawala wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo akitoa mwongozo kwa wananchi wakati wa mkutano huo
Mfanyabiashara ya Nyanya akipanga bidhaa hiyo katika soko la Kigogo Fresh, Pugu kabla ya mkutano huo kuanza
Baadhi ya wananchi wakiwa wamejikinga jua kwa nguo, wakati wa mkutano huo
Katibu wa Tarafa ya Ukonga, Jeremia Makorere akitoa maelezo ya awali kabla ya mkutano kuanza
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kigogo B, Mariano Maurus akizungumza kwa naiaba ya wenyeviti wengine wa mitaa katika kata hiyo wakati wa mkutano huo
Mkuu wa Wilaya ya Ilala sophia Mjema akihutubia wananchi katika mkutano wa kutatua kero uliofanyika jana katika Soko la Kigogo Fresh, Pugu, Dar es Salaam, jana. Kulia ni Katibu tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo
Kina mama wafanyabiashara katika soko la Kigogo Fresh,Pugu wakimshangilia Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema wakati akihutubia kwenye mkutano huo
Wafanyabiashara katika soko la Kigogo Fresh wakimsikiliza Mkuu wa wialaya ya Ilala sophia Mjema wakati akihutubia mkutano huo
Baadhi ya bidhaa zikiwa zimetelekezwa na wafanyabiashara, waliokwenda kumsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, wakati wa mkutano huo
Baadhi ya wananchi waliojipanga kwa ajili ya kueleza kero na kuuliza maswali mbalimbali wakati wa mkutano huo wa mkuu wa wilaya sophia Mjema
Kijana mfanyabiashara katika soko la Kigogo Fresh akiuliza swali na kueleza kero zinazokabili soko hilo
Wananchi wakifuatilia wakati wa kutano huo kwenye soko la Kigogo Fresh
Mkazi wa Kigogo Fresh akipaza sauti wakati akieleza kero zinazokabili wananchi katika soko la Kigogo Fresh wakati wa mkutano huo
Moja ya stakabadhi zilizodaiwa kutolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa wafanyabiashara wa soko la Kigogo Fresh ambazo hazionyeshi, jina la mtoza ushuru wala jina la mlipaji ushuru au kizimba anacholipia ushuru, ambazo wafanyabiashara wa soko hilo walionyesha kutoziamini
Sehemu ya eneo la mam/babalishe katika soko la Kigogo Fresh
Mmoja wa wakazi wa Kigogo Fresh akielezakero wakati wa mkutano huo
Mkuu wa Wilaya ya Ilala sophia Mjema akijibu maswali na kero zilizoibuliwa na wananci wakati wa mkutano huo
Wananchi hasa kinamama wakimshangilia Mkuu wa Wialaya ya Ilala Sophia Mjema baada ya kugusa kero zao na kuzitatua ikiwemo ulipwaji ushuru katika soko la Kigogo Fresh, Pugu huku miundombinu ya soko hilo ikiwa haijakamilishwa vya kutosha. Mkuu wa wilaya amesimamisha ulipwaji wa uhsuru huo hadi januari mwakani Halmashauri ya Ilala itakapokuwa imekamilisha miundombinu hiyo ya soko hilo.
Katibu Tawala waWilaya ya Ilala Edward Mpogolo akizungumza wakati Kinamama walipojitokeza kumzawadia Mama Mjema Nyanya baada ya kufurahishwa na hotuba yake.
Kina mama wakimzawadia Mama Mjema zawadi ya Nyanya
Kinamama akimpongeza Mjema kwa kutatua kero zao katika sokola Kigogo Fresh
Mkuu wa wilaya ya Ilala sophia Mjema akiwaaga wananchi baada ya mkutano huo
Msafara wa Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema ukiondoka Kigogo Fresh, Pugu kwenda Gongolamboto kufanya mkutano mwingine wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi
Ofisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala Ndugu Tabu, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa hiyo
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo akisawazisha mambo kabla ya kuanza mkutano wa hadhara katika uwanja wa Kampala, Gongolamboto
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo
Wananchi wakiwa kwenye Uwanja wa Kampala, Gomgolamboto kwenye mkutano huo
Wananchi kwenye mkutano huo
Mmoja wa wananchi wa Gongolamboto akiuliza maswali na kuelezea kero mbalimbali zinazowakabili wananchi ambazo alidai nyingi zinasababishwa na mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Gongolamboto Bakari Shingo wa Chadema
Mwanadada Amina Omari akieleza kero ya maji
Mkuu wa Wilaya ya Ilala sophia Mjema akitoa majibu na utatuzi wa kero mwishoni mwa mkutano wa hadhara ya kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili wananchi katika Kata ya Gongolamboto, wilayani humo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni