Warembo 30 wanaoshiriki kinyanganyiro cha kumsala Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara tu baada ya kutembelea ofisi za gazeti la Guardian zilizopo ndani ya mkoa wa Arusha |
picha ikionyesha baadhi ya warembo akiwemo mwenyeji wao ambaye ni miss Arusha wa pili kulia Maurine Ayubu wakiwa ndani ya ofisi za gazeti la Gurdian na Nipashe zilizopo jiji Arusha
Msimamizi wa kituo cha Gazeti la Gurdian na Nipashe mkoa wa Arusha na
Manyara Edward Qorro akiwa anatoa maelekezo mafupi kwa warembo juu ya
kazi zinazofanya na magazeti hayo katika mkoa huu
warembo ndani ya ofisi
Msimamizi
wa kituo cha Gazeti la Gurdian na Nipashe mkoa wa Arusha na Manyara
Edward Qorro akipokea mkoa wa Shukrani kutoka kwa Mshiriki wa mashindano
ya miss Tanzania kutoka mkoa wa Arusha Maurine
Ayubu ambaye pia ndio mshindi wa Miss kanda ya kaskazini mara baada
yakumaliza kutmbelea ofisi za magazeti hayo zilizopo apa Arusha
mkuu wa kituo siaakaamua kutumia mda huo kuji selfie na warembo
Meneja masoko wa gazeti la Gurdiaan Swalehe Walii akiwa anatoa zawadi ya soda kwa mrembo Maurine Ayubu ambaye ni mwenyeji wa warembo wenzake wanaoshiriki shindano hilo kwani ametokea mkoa wa Arusha
warembo wakiwa wanatoka katika ofisi za gazeti la The gurdian mara baada ya kumaliza kutembelea
nilipata
wasaa wa kupiga picha na baadhi ya wakuu wa msafara wa warembo hao wa
kwanza kabisa ni kulia mimi mwenyewe mmiliki wa blog ya libenele la
kaskazini woinde shizza akifuatia akifuatiwa Mshiriki wa mashindano ya miss Tanzania kutoka mkoa wa Arusha Maurine
Ayubu ambaye pia ndio mshindi wa Miss kanda ya kaskazini,wa pili
kushoto ni muuandaaji wa shindano la mss kanda ya mashariki Alex
NIkitas
warembo wakitoka ndani ya ofisi za The Gardian na nipashe zilizopo mkoani Arusha
Habari picha na Woinde Shizza,Arusha
Jumla ya
warembo 30 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchi ni wanashiriki shindano
la kumsaka mrembo wa Tanzania (Miss Tanzania) leo wameingia Rasmi mkoani
Arusha na kutembelea ofisi za gazeti la The Guardian na Nipashe ikiwa
ni moja ya kazi ambazo watazifanya wakiwa mkoani hapa.
Akizumza na waandishi wa habari Mkuu wa Itifaki wa
Miss Tanzania Albert Makoye alisema kuwa wameingia jijini hapa leo na
wanakaa kwa muda wa siku tatu ,na katika siku hizo wanampango wa kufanya
shughuli mbalimbali za kijamii
Aidha alisema
kuwa pia ndani ya siku hizo tatu kutakuwa nashindano la Top model ambalo
litafanyika Jumamosi October 15 katika ukumbi wa Triple A ulipo ndani
ya jiji la Arusha
"tunafanya
shindano hilo katika ukumbi wa triple A natunarajia wananchi wengi wa
Arusha watajitokeza kuwaona warembo hawa na kiingilio cha shindano hilo
ni shilingi 10000 tu hivyo napenda kutumia mda huu kuwaalika wananchi wa
Arusha kuja kumuangalia nani atakuwa Top Model"alisema Makoye
Alisema kuwa
mbali na hapa warembo hao wameshatembelea mikoa mbalimbali ikiwemo Mkoa
wa Dodoma,Singinda ,Dar es Salaam hapa Arusha na hatimaye wanatarajia
kuondoka na kwenda mwanza ambapo ndipo shindano hili linafayanyika kwa
mwaka huu .
Alisema kuwa
shindano la Miss Tanzania linatarajiwa kufanyika october 29 katika
ukumbi wa Rock City Mall ambapo alibainisha adi sasa warembo wote 30
wapo vizuri na wanasubiria siku yenye ifike na maandalizi yashindano
yamekamila
Kwa upande wake mkuu wa kituoa cha The Gardian /Nipashe mkoa wa Arusha na Manyara Edward
Qorro alitoa shukrani kwa warembo hao kuwatambelea na kuwatakia kila la
kheri katika mashandano hayo wanayotarajia kushiriki hivi karibuni
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni