Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya (kushoto) akibadilishana mawazo na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) mara baada ya kuwasili ofisini kwake. Lengo la ziara ya balozi huyo lilikuwa ni kuelezea nia ya serikali ya India katika uwekezaji kwenye sekta ya gesi nchini.
Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya (kushoto) akisaini kitabu cha wageni. Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya akielezea uzoefu wa nchi ya India kwenye uwekezaji wa uzalishaji umeme kwa kutumia gesi asilia.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akiongoza kikao na Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya pamoja na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji Nchini(EWURA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA).
Sehemu ya watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani)
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo katika kikao hicho.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya (kushoto).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni