ABIRIA WANUSURIKA AJALI NDOGO YA NDEGE ARUSHA


WATU WATANO WAMENUSURIKA KIFO BAADA YA NDEGE WALIYOKUWA WANASAFIRIA KUTOKA KATIKA UWANJA MDOGO WA NDEGE WA ARUSHA KUPATA HITILAFU KWENYE INJINI YAKE MUDA MFUPI BAADA YA KURUKA NA KUMLAZIMU RUBANI KUTUA KWENYE SHAMBA LILILOKO KARIBU NA UWANJA HUO  BAADA YA KUSHINDWA KUIFIKISHA UWANJANI
 

KAIMU MENEJA WA UWANJA WA NDEGE WA ARUSHA BW, BASHIRU JUMA AMESEMA AJALI HIYO IMETOKEA SAA SITA NA DAKIKA HAMSINI NA TANO JANA IKIWA NI DAKIKA TANO TU BAADA YA KURUKA IKIWA NA ABIRIA WANNE NA RUBANI MMOJA IKIWA INATOKA KWENYE UWANJA HUO KWENDA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA KIMANJARO
 

KWA MUJIBU WA BW BASHIRU, AJALI HIYO YA NDEGE AINA YA CARAVAN 5H ZEB YA KAMPUNI YA COASTAL AIR HAIKULETA MADHARA NA ABIRIA WOTE PAMOJA NA RUBANI WAMETOKA SALAMA NA PIA HAKUNA UHARIBIFU WOWOTE UNAOONEKANA KWA MACHO KWENYE NDEGE HIYO NA KWAMBA TARATIBU VYOMBO VINAVYOHUSIKA NA MASUALA YA ANGA KUCHUNGUZA TUKIO HILO ZINAENDELEA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni