Daniel Sturridge amefunga mara mbili
wakati Liverpool ikiitoa Tottenham kwa magoli 2-1 na kutinga robo
fainali ya kombe la EFL, na kuweka rekodi ya kutofungwa katika
michezo 10.
Sturridge ambaye jumamosi aliingia
akitokea benchi katika mchezo walioifunga West Brom, jana ilimchukua
dakika 10 tu kufunga goli kwa shuti la umbali wa yadi sita.
Divock Origi aliyeonyesha kiwango
kizuri alimtengenezea nafasi mbili Sturridge ambaye alizipoteza,
lakini baadaye wawili hao walishirikiana vizuri na Sturridge kufunga
goli la pili.
Daniel Sturridge akifunga goli la kwanza la Liverpool
Mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge akifunga goli la pili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni