Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amekebehi uvumi wa hivi karibuni kuhusu afya yake, kwa kusema kwa mzaha kwamba alikufa na kisha kufufuka.
Mugabe, 92, ametoa kauli hiyo ya mzaha, wakati alipowasili kutoka nje katika uwanja wa ndege wa Harare akiwa kwenye hali ya uchangamfu wakati akishuka kwenye ndege.
Safari yake ya ndege ilikuwa ielekea Asia ya Mashariki, lakini badala yake alienda Dubai, ambapo amesema alienda huku kwa masuala ya kifamilia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni