RAIS KENYATTA ASEMA KENYA NA TANZANIA HAZINA MGOGORO WOWOTE

Rais Uhuru Kenyatta leo amepuuzia ripoti za vyombo vya habari vya Kenya zinazoashiria kuwepo kwa mgogoro baina ya Kenya na Tanzania.

Akiongea wakati akizindua temino ya pili katika bandari ya Mombasa, rais Kenyatta amekanusha kuwepo kwa aina yoyote ya mgogoro, na kusema nchi hizo zinategemeana.

Nimesoma magazeti na kuangalia televisheni zikiashiria kuwepo mgogoro baina yetu, lakini nataka kuwaeleza wazi kuwa Kenya na Tanzania hazipo kwenye mgogoro wa aina yoyote,” alisema Kenyatta.

Rais Kenyatta amesema uchumi wa mataifa haya mawili unaingiliana na ni kwa manufaa ya wananchi wa Kenya na Tanzania.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni