SUZA YAWA MWENYEJI WA CHAWAKAMA

 Wanahabari kutoka vyombo vya Habari mbali mbali nao hawakuwa nyuma katika ushiriki kwenye Kongamano.
 Viongozi wakiwa katika meza kuu wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo. Mgeni rasmi Mheshimiwa Rashid Ali Juma (wa tatu kulia), Waziri wa Habari, Michezo, Utamaduni na Sanaa akibadilishana na Bwana Abdalla Mwinyi Khamis (aliyevaa kofia), Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi mstaafu.
 Mheshimiwa mgeni rasmi, viongozi mbali mbali na washiriki wa Kongamano wakati wa zoezi la kupandisha bendera za nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuashiria ufunguzi rasmi
          Washiriki wa Kongamano kutoka mataifa wanachama wa CHAWAKAMA.

Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kimekuwa mwenyeji wa Kongamano la 12 la Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili wa Afrika ya Mashariki (CHAWAKAMA) ambalo limeanza tarehe 21 Septemba, 2016 na kufunguliwa na mgeni rasmi Mheshimiwa Rashid Ali Juma, Waziri wa Habari, Michezo, Utamaduni na Sanaa. Kongamano hili ambalo litafungwa tarehe 23 Septemba, 2016 linafanyika katika ukumbi wa jengo la zamani la Baraza la Wawakilishi ambao sasa ni la Wizara ya Habari, Michezo, Utamaduni na Sanaa.

Katika Kongamano hili lenye kauli mbiu “Kiswahili chako, fursa yako” linaambatana na utoaji wa mada kutoka kwa wataalamu mbali mbali wa lugha ya Kiswahili na kuwa na majadiliano yanayohusu lugha ya Kiswahili pamoja na mila, silka, tabia, desturi na utamaduni unaoambatana na lugha hiyo. K wa hisani ya ZanziNews

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni