Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadiq akipokea salamu za heshima
kutoka kwa askari wakati wa gwaride maalum lililoandaliwa wakati wa
hafla fupi ya kutunuku zawadi kwa askari 34 wa vyeo mbalimbali
waliotekeleza vyema majukumu yao.kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kilimanjaro ,Wilbroad Mutafungwa.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Saidiq akikagua gwaride la heshima
baada ya kuwasili katika viwanja vya kikosi cha kutuliza ghasia mjini
Moshi kwa ajili ya hafla ya kuwapongeza na kutunuku zawadi kwa asakari
34 waliotekeleza vyema majukumu yao.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Saidiq akihitimisha ukaguzi wakati wa
gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili ya kuwapongeza asakari
walitekeleza vyema majukumu yao.
Ofisa
Mnadhimu wa jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Koka Moita akizungumza
wakati wa hafla ya kuwapongeza na kutunuku zawadi kwa asakari 34 wa
jeshi hilo waliotekeleza vyema majukumu yao.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa akizungumza wakati wa
hafla ya kukabidhi zawadi kwa askari 34 waliotekeleza vyema majukumu
yao.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadiq akizungumza wakati wa hafla ya
kuwapongeza na kutunuku zawadi kwa asakari 34 waliotekeleza vyema
majukumu yao.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa akimuoneesha Mkuu wa
Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadiq baadhi ya silaha zilizokamatwa hivi
karibuni zikidaiwa kutumika katika vitendo vya uharifu.
Mkuu
wa Kitengo cha dawa za kulevya cha jeshi la Polisi mkoa wa
Kilimanjaro,Mkaguzi wa Polisi,Ezekiel Midala akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro sehemu ya dawa za kulevya zilizokamatwa na jeshi hilo.
Baadhi ya askari waliotunukuwa zawadi kwa utendaji kazi mzuri wakisonga mbele kwa ajili ya kutunukiwa zawadi.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadiq akitunuku zawadi kwa baadhi ya
askari waliofanya vizuri katika kutekeleza majukumu yao.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Utalii ya Asante Tours ,Cuthbert Swai akizungumza wakati
wa hafla ya kuwapongeza na kutoa zawadi kwa asakari waliofanya vizuri
wakati wa kutekeleza majukumu yao.
Pikipiki
mbili aina ya Fekon zilizotolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya
Asante Tours ,Cuthbert Swai kusaidia jeshi la Polisi katika kutekeleza
majukumu yake ya kila siku.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadiq akiwa ameketi juu ya pikipiki
na kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishana Mwandamizi Msaidizi
wa Polisi,Wilbroad Mutafungwa wakati wa hafla ya kuwapongeza na kutoa
zawadi kwa askari 34 wa jeshi hilo mjini Moshi.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadiq akitoa cheti kwa Mkurugenzi wa
kampuni ya Ibraline ,Ibrahim Shayo akitambua mchango wa wadau kwa jeshi
la Polisi.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni