Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama Msaada wa tani mbili na nusu za mchele na mablanketi 100 vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 10 ukiwa ni msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Septemba 19, 2016. Kulia ni Meneja wa Uwekezaji wa Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation, Bw. Le Tong, Wapili kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Urafiki Kati ya Tanzania na China, Joseph Kahama, na wapili kushoto ni Afisa Uhusiano wa taasisi hiyo, Nice Munissy. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kaassim Majliwa akipokea msaada wa mgodoro 200 yenye thamani ya sh. 6, 000,000 kutoka kwa Bi. Anna Jiang wa Kampuni ya Chang Qing Inernational Investiment Limited ya nchini ukiwa ni msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwake jijjini Dar es salaam Septemba 19, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya sh. milioni 10 kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya EXIM, Bw. George Shumbusho (watatu kulia) ukiwa ni msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 19, 2016. Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Uledi Mussa, Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu wa Benki hiyo, Fredrick Kanga, wapili kushoto ni Chief Finance Officer wa benki hiyo, Selemani Ponda na watatu kushoto ni Meneja Masoko wa benki ya Exim, Abdul Nkondo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni