Basi la abiria pamoja lori la mafuta yamegongana kusini mwa Afghanistan, na kusababisha vifo vya watu 36.
Basi hilo lilikuwa likisafiri kutoka Kandahar kwenda Kabul wakati ajali hiyo ikitokea katika eneo la Jildak mkoani Zabul.
Wengi waliokufa, wamo wanawake na watoto, ambapo watu wameungua kiasi cha kushindwa kutambulika. Watu wengine 25 pia wamejeruhiwa.
Nchi ya Afghanistan imekuwa na ajali mbaya za barabarani, ambapo barabara nyingi ziko katika hali mbaya na magari ni mabovu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni