Katika
kile ambacho wasanii wanakiita 'kutafuta kiki', au kutaka umaarufu wa
haraka, mwanamuziki mmoja nchini Jamaica amefanyiwa operesheni na
kuwekewa pembe mbili kichwani.
Msanii huyo anayejulikana kama Furtyle Brain, amefanyiwa operesheni hiyo katika hospitali moja nchini Canada kwa kulipa kiasi kikubwa cha pesa.
Na ingawa anasema yeye si muumini wa shetani, lakini muonekano wake wa sasa kichwani unamuonyesha kama shetani kwa pembe zake mbili zilizochomoza usawa wa utosi wa kichwa chake.
Brain amesema licha ya kupata maumivu makali wakati wa kufanyiwa operesheni hiyo, kwa kutobolewa fuvu la kichwa, bado mpaka sasa anapata maumivu pale anapolala vibaya na kuzikandamiza pembe zake, lakini amesema anafurahia sana muonekano wake wa sasa.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni