SERIKALI YAAHIDI MAZINGIRA SALAMA KWA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU.

Afisa Tawala Wilaya ya Nyamagana, Kombe Danty (wa pili kushoto), akizungumza kwenye ungaji wa Mafunzo/Semina ya Utetezi wa Haki za Binadamu katika Sekta ya Madini nchini hii leo jijni Mwanza. Na George Binagi-GB Pazzo

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Mary Tesha, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Watetezi wa Haki za Binadamu nchini ikiwemo kuweka mazingira salama katika utendaji wao wa kazi.

Tesha ameyasema hayo hii leo Jijini Mwanza, katika hotuba yake iliyosomwa na Afisa Tawala Wilaya ya Nyamagana, Kombe Danty, kwenye ungaji wa Mafunzo/Semina ya Utetezi wa Haki za Binadamu katika Sekta ya Madini nchini.

Naye Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa, amesema mtandao huo umekuwa ukitoa semna kwa watetezi mbalimbali wa haki za binadamu ili kuwajengea uwezo wa kufanya kazi bila migogoro yoyote na serikali.

Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Heri Nkoromo, Afisa Tawala Wilaya ya Nyamagana, Kombe Danty, Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa na Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu mikoa ya Mara, Mwanza na Simiyu, Antony Mayunga.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Heri Nkoromo, akizungumza kwa niaba ya mbunge huyo, ambapo amewasihi washiriki wa mafunzo hayo kufikisha elimu waliyoipata kwa watetezi wengine ambao hawakubahatika kuhudhuria semina hiyo.
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa (kulia), anasema wakati mwingine Watetezi wa Haki za Binadamu wamekuwa wakichukuliwa kama wachochezi kwenye jamii jambo ambalo si sahihi.
Washiriki wa Semina hiyo ya siku tatu, iliyoanza Agosti 31,2016 wamepatiwa vyeti vya ushiriki ambapo pichani ni Jimmy Luhende kutoka taasisi ya Utawala Bora nchini, akipokea cheti cha ushiriki.
Angel Benedict kutoka Shirika la Kutetea Wafanyakazi wa Majumbani, Wote Sawa, la Jijini Mwanza, akipokea cheti cha Ushiriki.
Mwanahabari na Mwendeshaji wa Mtandao wa Mabadiliko Forums, akipokea Cheti cha Ushiriki.
                                                                        Mshiriki akipokea cheti cha Ushiriki
                                                                      Mshiriki akipokea cheti cha Ushiriki
                                                                       Mshiriki akipokea cheti cha Ushiriki
                                                                          Mshiriki akipokea cheti cha Ushiriki
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini (THRD) unajumuisha Watetezi/Watu wanaotetea haki mbalimbali katika jamii ikiwemo kwa makundi ya Wakulima, Wafugaji, Waandishi wa Habari, Wanasheria, Katiba, Utawala Bora, Watoto, Wanawake miongoni mwa makundi mengi katika jamii.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni