HOSPITALI YA KISASA YA MUHIMBILI-MLOGANZILA KUANZA KUTOA HUDUMA JANUARI 2017.

UJENZI wa Hospitali ya kisasa ya kufundishia wataalamu wa afya na kutoa huduma -shirikishi ya Muhimbili iliyopo Mbezi eneo la Mloganzila jijini Dar es Salaam yakaribia kumalizika kufunga vifaa tiba na kuanza kufanya kazi ifikapo Januari 2017 itaanza kutoa huduma mbalimbali  kwaajili ya kufundishia fani za afya na kutoa huduma ya matibabu yapasayo kwa wagojwa.

Hayo yamesemwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi cha Muhimbili, Profesa Ephata Kaaya wakati waandishi wa habari  walipotembelea katika hospitali hiyo ya kisasa ya kufundishia wataalamu wa  afya na kutolea huduma mbalimbali za afya hapa nchini.

Amesema kuwa eneo la hospitali hiyo linaukubwa wa ekari 3800 na inauwezo wa kuchukua vitanda 571 na ipo umbali wa Kilomita 25 kutoka jijini Dar es Salaam pia inauwezo wa kuchukua wanafunzi 4000 ikitofautishwa na waliopo sasa ni 1500 tuu.

 Profesa Kaaya amesema kuwa upungufu wa wataalamu wa afya katika mikoa na wilaya hapa nchini ndiko kulikosababisha  Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi ya Muhimbili kuanza kutafuta maeneo yakupanua na kujenga hospitali ya Kisasa ya kufundishia wataalamu wa afya na kutoa huduma za afya.

Profesa Kaaya amesema kuwa wagojwa watakaopelekwa katika hospitali hiyo ni wale watakaokuwa wamepewa rufaa kutoka hospitali za mikoa mbalimbali ya hapa nchini.

Amesema kuwa jengo hilo lina sehemu mbili na linaghorofa tisa za juu na ghorofa moja chini ya ardhi linaeneo la Mapokezi, Idara ya Utawala, Idara ya Mahesabu, Phamasia, Idara ya Mionzi, Idara ya wagonjwa wa dharula pamoja na upasuaji wa Dharala, Idara ya afya ya kinywa na meno,chumba cha wagojwa  mahututi, chumba cha kusafisha figo na wadi ya kujifungulia.
Eneo jingine ni vyumba vya kufundishia wanafunzi maktaba ya hospitali, ofisi ya mkuu wa hospitali, ofisi za madaktari na waalimu, ofisi ya Muuguzi Mkuu na kituo cha kopyuta.
 Mwonekano wa Jengo la Hospitali ya Kisasa ya kufundishia wataalamu wa afya na kutoa huduma za afya.




Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi cha Muhimbili, Profesa Ephata Kaaya akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea katika Hospitali ya Kisasa ya kufundishia wataalamu wa afya na kutoa huduma za afya jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Makamu Mkuu wa chuo Kikuu cha Afya na Sayansi cha Muhimbili, Dkt. Said Aboud.

 Baadhi ya Madaktari na wakuu wa vitengo wa Hospitali ya Kisasa ya kufundishia wataalamu wa afya na kutoa huduma za afya wakiwa katika mkutano jijini Dar es Salaam leo.
 Mkandarasi kutoka Korea  kusini Kulia akitoa maelekezo jinsi jengo la Hospitali ya kisasa ilivyo.
Mhandisi Umeme katika jengo la hospitali ya kisasa, Omary Killo akitoa maelekezo mara baada ya kutembelea katika mitambo ya umeme ya jengo hilo. 
 
Baadhi ya Mitambo ya kusafishia maji katika jengo la hosptali hiyo ya kisasa.
Mtaalamu wa Tehama, Andrew Fundamali akitoa maelekezo kwa waandishi wa habari walipotembelea katika mitambo ya tehama katika hospitali hiyo.
 Mwongozaji akitoa maelekezo kwenye chumba cha Kufulia nguo pamoja na kunyoosha katika hosptali hiyo leo.
 Wandishi wakipewa maelekezo walipotembelea katika chumba chenye mashine za MRI na CT scan.
 Daktari bingwa wa Tiba ya Dharula, DK. Hendry Sawe akitoa maelekezo kwa waandishi wa habari walipotembelea chumba cha Dharula.
 Baadhi ya Vitanda vya wagonjwa vilivyopo katika hospitali hiyo.
 Daktali wa kitengo cha Koo, pua na masikio akitoa maelekezo kwa waandishi wa habari.
 Naibu Makamu Mkuu wa chuo Kikuu cha Afya na Sayansi cha Muhimbili na mkuu wa maabala Dkt. Said Aboud akitoa maelekezo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
 waandishi wakipata maelekezo.
 Mkufunzi wa chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi ya Muhimbili, Paschal Ruggajo akitoa maelekezo kwa waandishi wa habari walipotembelea katika wodi ya wangojwa mabalimbali katika jengo la Mloganzila.
 Mkufunzi wa chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi ya Muhimbili, Wangwe Peter akitoa maelekezo.
 Eneo la Gesi.
Eneo la Majenereta.
 Jengo la hospitali ya Afya na Sayansi shirikishi ya Muhimbili ya Mloganzila muonekano wake kwa nyuma.
 Mwonekano wa Jengo hilo kushoto ukiwa mbele ya jengo hilo.  
Mwonekano wa Jengo hilo kwa mbele.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni