Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa tai)
akielekea Stendi Kuu ya Mabasi ya mikoani Ubungo, jijini Dar es Salaam
wakati alipofanya ziara ya kushtukiza yenye lengo la kukagua mabasi
mabovu pamoja na usalama wa abiria katika Stendi hiyo pamoja na Stendi
ya Kibaha mkoani Pwani. Masauni alilizuia Basi la Shambarai lenye namba
za usajili T419 BUF na Basi la Karachani (T253 CLZ) ambayo yalikuwa
yanaenda Tanga kutokuendelea na safari zake kutokana na ubovu wa mabasi
hayo ambayo yangeweza kuhatarisha maisha ya abiria. Kushoto ni Mkuu wa
Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwauliza
abiria wa Basi la Harambee linalofanya safari zake Dar es Salaam kwenda
Arusha, maswali mbalimbali kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo wakati
wanaposafiri. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya
Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu
wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed
Mpinga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akikagua
mikanda katika Basi la Shambalai wakati alipofanya ziara ya kushtukiza
katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es
Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto)
akioneshwa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu
Kamishna, Mohamed Mpinga, tairi la Basi la Shambalai ambalo halina ubora
kwa ajili ya kusafirisha abiria. Hata hivyo Masauni aliagiza basi hilo
lizuiwe kufanya safari na pia kuchukuliwa hatua kali kwa Mmiliki wa basi
hilo pamoja na Dereva. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa tai)
akizungumza na madereva wa Basi ya mikoani pamoja na wa magari madogo
ya mizigo yanayopaki Stendi Kuu Ubungo, jijini Dar es Salaam. Masauni
aliwataka madereva hao kufuata sheria za usalama barabarani. Hata hivyo,
madereva hao walilalamika kuwa hawana mikataba ya kazi zao. Masauni
alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi hiyo, leo. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na waandishi wa habari, Picha ya Ndege Kibaha, Pwani, mara baada ya kukamilisha ziara yake ya kukagua mabasi mabovu na usalama wa abiria. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam pamoja na Kibaha mkoani Pwani leo. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, Bonaventura Mushongi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto)
akihoji usalama wa mtoto baada ya kugundua siti moja kukaa watoto wawili
jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa abiria. Masauni alifanya ziara ya
kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini
Dar es Salaam. Na baadaye alielekea Stendi ya Kibaha kuendelea na
ukaguzi huo wa mabasi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto)
akiwasalimia wananchi wa Picha ya Ndege, Kibaha mkoani Pwani mara baada
ya kumaliza ukaguzi wa mabasi mabovu pamoja na madereva ambao hawana
leseni. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi
yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam. Na baadaye alielekea
Stendi ya Kibaha kuendelea na ukaguzi huo wa mabasi. Picha zote na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni