Mtawa Mama Teresa, ambaye anajulikana zaidi kwa kujitolea katika kuwasaidia masikini nchini India, atatangazwa kuwa mtakatifu hii leo Jijini Vatican.
Makumi kwa melfu ya watu wamekusanyika katika eneo lawazi la Kanisa la Mtakatifu Peter kushuhudia Papa Francis akiongoza hafla hiyo ya kutangazwa Mtakatifu Mama Teresa.
Kuridhiwa utakatifu wa Mama Teresa kunafuatia ushuhuda wa miujiza miwili ya kutibu wagonjwa aliyofanya Mama Teresa, baada ya kifo chake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni