Timu ya Liverpool imeibuka na
ushindi wa magoli 5-1 dhidi ya Hull City katika mchezo wa Ligi Kuu ya
Uingereza ulioshuhudia Ahmed Elmohamady akitolewa nje kwa kadi
nyekundu na kuiathiri Hull.
Katika mchezo huo Liverpool walikuwa
wa kwanza kufunga goli kupitia kwa Adam Lallana na kuachia shuti
lililotinga kwenye eneo la juu la kona ya goli, kisha James Milner
akifunga la pili kwa penati baada ya Elmohamady kucheza rafu na
kupewa kadi nyekundu.
Sadio Mane aliongezea goli la tatu
akimalizia vyema kazi nzuri ya Lallana, huku Hull wakichomoa goli
moja kupitia David Meyler. Philippe Coutinho aliongeza la nne na
kisha James Milner kufunga kwa penati la tano baada ya Daniel
Sturridge kuangushwa.
James Milner akiifungia Liverpool goli kwa mkwaju wa penati
Mpira uliopigwa na Philippe Coutinho ukielekea kutinga wavuni na kuandika goli
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni