Wanawake wanne wapigwa risasi na
kufa na mwanaume mmoja amejeruhiwa vibaya katika eneo la maduka huko
Burlington, katika jimbo la Washington nchini Marekani.
Polisi wametoa picha ya mtu
anayetuhimiwa kufanya tukio hilo ambaye aliondoka kwenye eneo la
tukio akiwa na bunduki aina ya rifle.
Jengo la duka la The Cascade Mall
pamoja na maduka ya karibu watu wameondolewa na polisi wamewataka
wananchi kukaa mbali. Bado haijafahamika sababu ya shambulio hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni