MTALII AUWAWA KWAKUKANYAGWA NA TEMBO WAKATI AKIMPIGA PICHA



Mtalii raia wa Italia ameuwawa kwa kukanyagwa na tembo wakati akimpiga picha kwenye mbuga ya wanyama ya taifa ya Tsavo nchini Kenya.

Mtalii huyo Fernando Mocclola 66, walikuwa wamefikia kwenye kambi ya Swara ambako tukio hilo lilipotokea jana majira ya saa tano asubuhi.

Polisi wamesema mtalii huyo alimuacha mkewe akiwa kwenye hema na kwenda kuwapiga picha tembo waliokuwa wakinywa maji kwenye mto Sabaki.
                                                      Moja ya hema lililopo kwenye mbuga ya Tsavo 
                                                  Kundi la tembo likinywa maji kwenye mto Sabaki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni