MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA ARUSHA APANDISHWA KIZIMAMBANI KWA KUJIFANYA AFISA USALAMA


Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha Lengai Ole Sabaya akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kupewa dhamana
mwenyekiti wa UVCCM akiwa anatoka mahakamani mara baada yakupewa dhamana


Na Mahmoud Ahmad,Arusha
Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha  imemsomea mashtaka mawili Mwenyekiti wa umoja wa vijana (UVCCM) Lengai Ole Sabaya ambaye pia ni diwani wa kata ya Sambasha Wilaya ya Arusha vijijini  .

Miongoni mwa makosa hayo aliyosomewa mahakamani hapo kosa la kwanza alituhumiwa kujifanya Afisa mtumishi wa serekali (TISS)huku kosa la pili ikiwa kugushi moja ya nyaraka za serekali(kitambulisho ).
Akisoma mashtaka hayo mahakamani hapo  Wakili wa serekali Lilian Mmasi  alisema kuwa Mnamo  May 18 katika hotel ya Skyway  iliopo makao mapya jijini Arusha Mshitakiwa alijitambulisha kama Afisa utumishi  wa  idara ya usalama wa taifa na kufanya Utapeli .
Wakili Mmasi alitaja kosa la pili ambalo Mshitakiwa Lengai Ole Sabaya alisomewa kuwa ni kugushi kitambulisho cha idara ya usalama wa Taifa  kilichokuwa kikisomeka jamuhuri ya muungano wa Tanzania idara ya usalama wa Taifa (TISS) Lengai Ole Sabaya kikosi maalumu Agent (undercover)chenye code no MT 86117 huku akitambua kuwa  ni kinyume cha kisheria .

Hata  hivyo mara baada ya kusomewa mashtaka hayo mahakamani hapo mtuhumiwa alikana mashtaka ndipo Hakimu Mkazi aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Gwantwa  Mwamkuga Alisema dhamana ipo wazi iwapo wathamini watakithi vigezo vinavyotakiwa na mahakama hiyo.

Hata hivyo Mshitakiwa alipata dhamana baada ya kukithi vigezo vilivyowekwa na mahakama ambapo ilikuwa ni wadhamini wawili wenye sifa ambapo kwanza awe mtumishi wa serikali pili awe na mali isiyohamishika yenye thamani ya shilingi milioni tatu kwa kila mmoja.
 Kesi imeairishwa na hakimu  mkazi hadi itapotajwa tena October 5  ambapo uchunguzi unatarajiwa kukamilika na kesi hiyo kuanza kusikilizwa.

Mara baada yakupata dhamana mahakamani hapo  wakili wa mtuhumiwa Yoyo Asubui alisema kuwa mshtakiwa amesomewa mashtaka yote mawili na kukana mashtaka ambapo wanatarajia uchunguzi ukikamilika  kesi itaanza kusikilizwa mapema na haki kutendeka ,huku akimtaka mteja wake kuendelea na majukumu ya mandeleo kwa wananchi wa kata ya Sambasha.

“kwakweli kesi hii sio ya kweli na naweza kusema ipo kisiasa na nashukuru  jeshi la polisi kwa kunishikilia na kukaa na mimi vyema hadi kunileta mahakamani ambapo naamini haki itatendeka na ukweli utabainika “Alisema Sabaya mara baada ya kupata dhamana

Alisema kuwa hili limetokea mara baada ya kuwatoa wabadhilifu wa mali za umoja wa vijana (UVCCM) ambapo kwa muda mrefu wamekuw a mali za umoja huo kujinufaisha wenyewe na vijana kukosa maendeleo kupitia miradi ya umoja huo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni