Msafara wa makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzani Samia Suluhu Hassani ambao ulikuwa unaelekea wilayani tandahimba ukitokea ikulu ndogo ya rais mtwara umepata ajali na kusababisha majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali ya rufaa Ligula.
Ajali imetokea mbele kidogo ya kijiji cha Nanguruwe kilichopo halmashauri ya wilaya ya Mtwara
Majeruhi walioumia ni dereva pamoja na wasaidizi wanne wa makamu rais.
Awali kabla ya gari hilo lililobeba wasaidizi wa rais kuacha njia na kupinduka, gari liliokuwa limebeba waandishi wa habari wa channel ten, startv na clouds tv liliacha njia na nusura kupinduka.
Barabara ya kutoka mtwara kuelekea tandahimba si ya kiwango cha kuridhisha na kuruhusu magari kwenda mwendokasi hali iliyosababisha magari hayo kuacha njia na moja kupinduka kabisa na kusababisha majeruhi.
Watu wanne wamejeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Mtwara, baada ya moja kati ya magari yaliyokuwa katika msafara wa Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hasssan Kupata ajali.
Ajali hiyo imetokea wakati Makamu wa Rais alipokuwa njiani kuelekea wilayani Tandahimba kutembelea kiwanda cha kubangua korosho cha Amama ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku tatu mkoani mtwara.

Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( Jwtz ) wakiangalia ndani ya gari aina ya Toyota Land Cruise baada ya kupata ajali.
Ajali hiyo imetokea katika eneo la Nanguruwe takribani kilomita 45 kutoka Mtwara mjini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni